Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, January 2, 2013

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI MUNDINDI WILAYANI LUDEWA AFARIKI DUNIA KWA AJALI

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mundindi Wilayani Ludewa Mkaoni Njombe Laurence Haule Amefariki na Wengine Kujeruhiwa Katika Ajali ya Pikipiki Zilizogongana Uso Kwa Uso Zenye Namba ya Uasjili T.  505 ATR Aina ya XGJAO na T.533 BCQ Aina ya Star.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Januari Mosi Mwaka Huu Majira ya Saa Saba Usiku  Katika Kijiji Hicho.

Acp Ngonyani Amewataja Majeruhi wa Ajali Hiyo Ambao Wamelazwa Katika Hospitali ya Lugalawa Wilayani Ludewa Kuwa ni  Goodluck Komba na Stephano Mlowe Wakazi wa Mundindi

Katika Hatua Nyingine Kamanda Ngonyani Amewapongeza Wananchi wa Mkoa wa Njombe Kwa Kusherehekea Sikuku za Mwisho wa Mwaka Kwa Amani na Kutii Sheria Bila Shuruti.
Hata hivyo kamanda huyo amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuendelea kutii sheria bila shuruti huku akisema watoe ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wanatokomeza vitendo vya ujambazi na udokozi katika maeneo jamii inapoishi  na kuishi kwa amani na utulivu na kuripoti matukio maovu katika vituo vya polisi vilivyopo jirani nao.

No comments:

Post a Comment