Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, January 1, 2013

DC LUDEWA JUMA MADAHA AWAPA SOMO LUDEWA


Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa  Juma Madaha  amewataka  watumishi  wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Ludewa  kufanya  kazi kwa upendo na mshikamano kama njia ya kuuanza mwaka mpya  wa 2013 kwa upendo na ufanisi zaidi.
Mkuu  huyo  wa  wilaya ametoa kauli  hiyo leo wakati wa kuwaaga watumishi wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa na kuwakaribisha  watumishi wapya pamoja na kuaga na kukaribisha mwaka mpya  wa 2013 ,sherehe  zilizofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya  wilaya ya Ludewa .

 Asema kuwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ni watumishi ambao wanaweza kulikomboa Taifa katika dimbwi la umasikini iwapo kama kila mtumishi atadumisha umoja na mshikamano .

 Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kila mtumishi ni lazima kujuwa wajibu wake na kutambua malengo yake katika kuitumikia Halmashauri hiyo ya wilaya ya Ludewa na kudai kuwa baada ya kugawanywa mkoa wa Iringa na Njombe hivi sasa mkoa wa Njombe ndio unapiga hatua zaidi katika maendeleo ukilinganisha na mkoa wa Iringa.

Aidha awataka watumishi wa Halmashauri ya Ludewa kuhakikisha wanafika kazini saa mmoja asubuhi na saa 1.30 kuanza kazi ya serikali badala ya kufika kazini kwa kuchelewa .

 Madaha alisema kuwa hakuna haki bila kutimiza wajibu na kuwataka watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutimiza wajibu kwanza katika kazi badala ya kudai haki bila kutimiza wajibu .

 Amtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Fidelis Lumato kuhakikisha anawabana watumishi wasiowajibika huku akiwataka watumishi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuzingatia sheria ,kanuni na utaratibu huku kuonyesha mfano mwema katika maeneo yao ya kazi.

 Madaha alisema kuwa hatakuwa na huruma kwa mtumishi wa Halmashauri hiyo atakayeshindwa kutimiza wajibu wake na kuwa kwa mwaka 2013 nyaraka zote za sheria za utumishi wa umma zitawekwa mahali ambapo kila mtumishi ataweza kusoma na kuzitambua zaidi ili pale anapokiuka kuwajibika kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu.

 Akemea vitendo vya rushwa katika maeneo ya kazi na kutaka watumishi kuchukua hatua ya kupambana na rushwa na kuwa rushwa katika wilaya ya Ludewa inapaswa kupigwa viti na kila mmoja .

 Mkuu huyo wilaya amesema kuwa iwapo kila mtumishi wa wilaya hiyo atafanya kazi kwa uaminifu na kuchukia vitendo vya rushwa wilaya hiyo itaendelea kupiga hatua katika maendeleo.

Kuhusu wastaafu mkuu huyo wa wilaya alitaka Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuweka utaratibu wa kuwasaidia wastaafu ili nao waweze kuendelea na kunufaika na matunda ya Taifa

 Alisema kuwa pamoja na wazee wastaafu kulitumikia vema Taifa ila bado maadili ya Taifa yameendelea kumomonyoka kutokana na wazee kushindwa kuwafunza vema vijana katika maadili mema na kuwa wazee waliowengi wanashindwa kuwalea watoto wao katika maadili kutokana na hali ya umasikini inayowakabili.

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akitoa  salam zake katika sherehe hizo alisema kuwa kwa upande  wake  amefarijika kufika katika sherehe  hizo na  kufanya  sherehe  hiyo ya kufunga mwaka na watumishi hao huku akieleza matumaini yake makubwa katika  kuwatumikia  wananchi wa jimbo la Ludewa. Chanzo: Gabriel Kilamlya
     

No comments:

Post a Comment