Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba aliyesimama akiwa na viongozi wengine akiwemo mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwin Mwanzinga .
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Leo Amezindua Rasmi Chanjo Mpya ya Magonjwa ya Nimonia na Kuhara Kwa Watoto Waliochini ya Umri wa Mwaka Mmoja.
Baadhi ya wazazi waliohudhuria katika uzinduzi wa chanjo ya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja
Akizungumza Kwenye Uzinduzi Huo Uliofanyika Kwenye Zahanati ya Idundilanga Mjini Njombe,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amesema Kutolewa Kwa Chanjo Hizo Zitasaidia Kupunguza Vifo Vya Watoto Waliochini ya Umri wa Mwaka Mmoja Ambao Wamekuwa Wakikumbwa na Magonjwa Hayo Mara Kwa Mara.
Katika Hatua Nyingine Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Wazazi na Walezi Wilayani Njombe Kuwapeleka Watoto Wao Kwenye Vituo Vya Afya Ili Waweze Kupatiwa Chanjo Hizo.
Muuguzi wa kituo cha afya Njombe Christina Ngongi akitoa maelezo juu ya chanjo hiyo kwa wazazi
Awali Akisoma Taarifa ya Chanjo Kwenye Uzinduzi Huo Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Pancrasi Ngulo Amesema Ili Kujikinga na Magonjwa Hayo Wananchi Wanapaswa Kuchukua Tahadhari Ikiwemo Kuishi Kwenye Nyumba Zinazoruhusu Hewa na Kujenga Vyoo Bora
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wazazi na Walezi Waliowapeleka Watoto Wao Kupatiwa Chanjo Hiyo Wameipongeza Serikali Kwa Hatua ya Kuanza Kutoa Chanjo Hizo
Kuzinduliwa Kwa Chanjo ni Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Serikali ya Tanzania Kwa Kushirikiana na Mashirika na Serikali Wahisani Ikiwemo Serikali ya Ujerumani Katika Kupunguza Vifo Vya Watoto Barani Africa.
No comments:
Post a Comment