Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, December 31, 2012



 JESHI LA POLISI NJOMBE LA HIMIZA AMANI NA UTULIVU.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limewataka Wananchi  Kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya Kwa Amani na  Kuendelea Kudumisha Amani Iliyopo.

Akizungumzia Hali ya Ulinzi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Jeshi Hilo Limejipanga Vyema Kuhakikisha Kuwa Amani Ina Kuwepo Ikiwa ni Pamoja na Kudhibiti Matendo ya Uvunjifu wa Amani.

Amesema Kwa Sasa Wamekuwa Wakifanya Doria za Mara Kwa Mara Katika Maeneo Yote ya Barabara Kuu Ikiwemo Kumbi za Burudani na Hivyo Kuwataka Wazazi Kuwa Makini Dhidi ya Watoto Wao.

Aidha Kamanda Ngonyani Ametoa Wito Kwa Kujihepusha na Vitendo Vinavyoweza Kuhatarisha Hali ya Ulinzi na Usalamaa Wakati wa Kusherekea Sikukuu ya Mwaka Mpya Ikiwemo Uchomaji wa Matairi Barabarani

No comments:

Post a Comment