Mbali na uharibifu huo, mvua hiyo pia imebomoa
madarasa sita ya Shule ya Sekondari Mnacho iliyoko katika Halmashauri ya
Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na jengo la utawala la shule hiyo.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zimeeleza
tukio hilo lililozua tafrani kwa wakazi wa eneo hilo, lilitokea juzi
katika Kijiji cha Ngau Chimbira B, kilichoko halmashauri ya Wilaya ya
Ruangwa.
“Uharibifu wote huo, ulitokea katika kipindi cha saa moja tu, ilipokuwa inanyesha mvua hiyo,” alisema mkazi wa eneo hilo Mwanaisha Seif.
“Uharibifu wote huo, ulitokea katika kipindi cha saa moja tu, ilipokuwa inanyesha mvua hiyo,” alisema mkazi wa eneo hilo Mwanaisha Seif.
Mkazi mwingine Issa Omari alisema mvua hiyo
ilianza kunyesha saa 9:00 hadi 10:00 jioni ikiwa inaambatana na upepo
mkali uliokuwa ikivuma kutoka Mashariki kwenda Magharibi.
Juma Said na Yohana Joseph, kwa nyakati tafauti wameeleza kwamba mvua hiyo iliyokuwa imeambatana na upepo mkali ilinyesha kwa takribani ya saa moja tu.
Juma Said na Yohana Joseph, kwa nyakati tafauti wameeleza kwamba mvua hiyo iliyokuwa imeambatana na upepo mkali ilinyesha kwa takribani ya saa moja tu.
Diwani wa kata ya Ngau Chimbira, Beda Mbila alisema nyumba 28 zimeezuliwa mapaa na kimbunga hicho.
Diwani huyo alifafanua kuwa kutokana na tukio hilo
waathirika wanahifadhiwa katika kwa ndugu na jamaa zao huku uongozi
ukiendelea kuangalia namna ya kuwasaidia zaidi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ruebern
Mfune amekiri kupata kwa taarifa ya tukio hilo, na kueleza bado hasara
iliyopatikana haijaweza kufahamika mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Agnes Hokororo alisema
ofisi yake imejipanga kushughulikia tatizo hilo kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali.
Kauli ya TMA
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini (TMA), Agnes Kijazi akizungumzia uharibifu huo alisema, hali hiyo ilitegemewa kwa kuwa utabiri uliotolewa na mamlaka hiyo Septemba mwaka huu, ulishaeleza hilo.

Kijazi alisema utabiri huo ulibainisha kuwa baadhi
ya maeneo ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, kutakuwa
na upungufu mkubwa wa mvua na maeneo ya Nyanda za juu Kusini Magharibi
katika mkoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa na Kanda ya Ziwa yatakuwa na mvua
nyingi zitakazoweza kusababisha uharibifu wa nyumba na mali.
No comments:
Post a Comment