Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, January 2, 2013

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE ASISITIZA WANANCHI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

Wananchi Wilayani Njombe Wametakiwa Kushirikiana na Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Katika Maeneo Yao Ili Kuondokana na Matukio ya Uhalifu Katika Kipindi Cha Mwaka 2013.

Aidha Halmashauri za Miji na Wilaya Nazo Pia Zimetakiwa Kusimamia Jukumu Lao la Kikatiba la Kusimamia Ulinzi na Usalama Kupitia Dhana ya Ulinzi Shirikishi Ambayo Imeanza Kuonesha Matunda Wilayani Hapa.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Bi Sarah Dumba Amesema Katika Kipindi Cha Mwaka 2012 Kumekuwa na Matukio Mengi ya Uhalifu Wilayani Njombe Ambayo  Kati Yan hayo Yamekuwa Yakisababishwa na Imani za Kishirikina na Kulipizana Visasi.

Ameongeza Kuwa Utekelezwaji wa Dhana ya Utii wa Sheria Bila Shuruti Miongoni Mwa Wananchi ni Njia mojawapo ya Kukabiliana na Matukio Hayo Wilayani Njombe.

No comments:

Post a Comment