Mvua Zinazoendelea Kunyesha Zikiambatana na Upepo Mkoani Njombe Jana Zimesababisha Uharibifu wa Zaidi ya Nyumba Tano Katika Eneo la Igeleke Mjini Njombe na Kusabaisha Baadhi ya Wakazi wa Nyumba Hizo Kuhifadhiwa Kwa Majirani.
Mvua Hiyo Iliyoanza Kunyesha Majira ya Saa Kumi Jioni na Kusababisha Hasara za Mali Mbalimbali Ambazo Hazijafahamika Thamani Yake
Akizungumza na Kituo Hiki Mwenyekiti wa Mtaa Kambarage Bwana Pankrasi Matinya Amesema Katika Tukio Hilo Hakuna Mtu Aliyefariki Huku Bwana Mgina Pamoja na Mtoto Wake Wakinusurika Kuangukiwa na Ukuta wa Nyumba Yao.
Aidha Bwana Matinya Amesema Tayari Jitihada za Kuwasaidi Wahanga wa Tukio Hilo Zimeanza Kuchukuliwa Kwa Mabalozi na Wananchi Kuchangia Fedha na Vifaa Vingine Kwa Ajili ya Kuwasaidia Wahanga Hao
Kwa Upande Wao Wananchi wa Mtaa wa Kambarage Wameshauri Kupandwa Miti Inayozuia Upepo Mkali Kuzunguka Maeneo ya Nyumba Zao.
Lakini pia mvua hizo zimeharibu nyumba moja katika mtaa wa posta kati mjini Njombe ambapo wananchi hadi sasa wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na mvua hizo.
No comments:
Post a Comment