Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, January 27, 2013

MANGULA AICHANGISHIA KWAYA YA FAITHA CHUO CHA TUMAINI IRINGA MILIONI 15


 wanakwaya wa Faith kutoka chuo kikuu cha tumaini wakiimba kabla ya harambee ya kuwachangia iliyoongozwa na makamu mwenyekiti Philip Mangula 
 Na Denis Mlowe wa  www.francisgodwin.blogspot.com,Iringa
Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa (bara ) Philip Mangula mwishoni mwa wiki aliongoza harambee ya kuchangia kwaya ya Faith ya CCT ya Chuo Kikuu cha Tumaini fedha za  kurekodi nyimbo zao za injili na video za nyimbo hizo.


Harambee hiyo lengo ilikuwa ni kupata kiasi cha sh. milioni 8 na kufanyika katika ukumbi wa Multirpose ulioko chuoni hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa ccm mkoa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati Mangula aliweza kuchangia kiasi cha pesa sh. Milioni 5 na watoto wake walichangia kiasi cha sh, laki 7 pesa ambayo aliikabidhi papo hapo na waziri wa fedha na uchumi Dr William Mgimwa alichangia kiasi cha sh. Milioni 5 na viongozi wengine waliochangia kiasi cha fedha ni pamoja na mwenyekiti wa ccm mkoa  Jesca Msambatavangu aliyechangia shilingi laki tano, Ritta Kabati laki 5 na kufanya jumla ya pesa yote kufikia zaidi ya milioni 15.


Aidha makamu mwenyekiti ki huyo kuonysha ni kiasi gani naye ni muimbaji mzuri aliweza kuimba wimbo "Tumshukuru mungu" wimbo ambao ulipokewa kwa shangwe na waliohudhuria harambee hiyo.
 “Nilikuwa mwanakwaya  na mwimbaji mzuri wakati wa ujana wangu na nilikuwa natumia sana chombo cha kitamaduni kiitwacho Mangala kwa ajili ya kumsifu MUNGU tukiwA pamoja na Askofu Mdegella” alisema Mangula

No comments:

Post a Comment