wanafunzi wa kidato cha 6 wa shule sekondari Iringa wakicheza kwaito wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. picha na denis mlowe
Mbunge wa Viti maalum Ritta
Kabati amewataka wazazi mkoani hapa kuchangia zaidi katika elimu na kuepukana
na tabia ya kuchangia zaidi katika sherehe kama harusi, ubatizo na mambo
mengine yasiyokuwa ya maana kwa lengo la kukuza zaidi elimu kwa watoto wa kike
Akizungumza katika mahafali
ya 13 ya kidato cha sita ya shule ya Sekondari ya Lugalo yaliyofanyika mwishoni
mwa wiki akiwa mgeni rasmi Ritta Kabati alisema kwamba wazazi wanatakiwa
kuwekeza katika elimu kwa mtoto wa kike kwa lengo kumkomboa kuondokana na
utegemezi uliokithiri katika jamii kwamba mtoto wa kike hana haki ya kupata
elimu.
“ Unapompeleka mtoto wa kike
shule ni sawa na kuikomboa jamii nzima katika kuleta maendeleo hivyo wazazi
changieni sana sana elimu kuliko mambo ya harusi mtaji wa masikini ni nguvu
zake mwenyewe hivyo hata kama we ni maskini wekeza katika elimu” alisema Kabati
Aidha alisema kwamba
kuchangia katika elimu ni mojawapo ya kuondokana na baadhi ya changamoto ambazo
hazihitaji serikali kutatua ni suala la wazazi kujitolea kwa uhakika katika
michango mbalimbali ya shule na kwa mtindo huo wa kuchangia katika elimu maendeleo yatakuja na kuweza kupunguza baadhi
ya changamoto zinazoikabili shule husika.
Kabati pia aliwata wazazi
wasiwe waoga katika kuwapatia elimu ya afya ya uzazi na ukimwi watoto wa kike
kwe lengo kupata jamii yenye mama bora na baba bora kuliko kuiachia serkili
kila jambo.
“tuwape elimu watoto lakini
tusisahau kuhusu janga la ukimwi linaloikabili jamii yetu hivyo wazazi msisite kuwapatia
elimu ya afya vijana wetu kujenga taifa lenye nguvu hapo” alisema Kabati
Katika mahafali hayo Ritta
Kabati alichangia simenti tani mbili sawa na mifuko 40 ikiwa na thamani ya laki
6 na 5 simenti kwa lengo la kujengea choo cha shule na kuahidi kuwapatia baadhi
ya komputa ambazo hakutaka kutaja idadi na alifanya harambee ya papo kwa hapo
na kufanikiwa kupata kiasi cha laki 6.5
Wanafunzi walifanikiwa hadi
sasa katika kumaliza kidato cha 6 katika shule hiyo ni 129 katika ya139 na kumi
kati yao walishindwa kuendelea kutokana na ugonjwa na wengine kuhama shule
alishuhudiwa mwanafunzi Malea Lusinde akijinyakulia ushindi jumla katika
taaluma na wa pili akiwa Shamira Msamba
No comments:
Post a Comment