Afisa mtendaji wa kata ya Ikuna bwana Job Fute akipiga marufuku biashara ya pombe asubuhi katika kijiji cha Matiganjola Jana.
Mamia ya wakazi wa kijiji cha Matiganjola wajitokeza kumsikiliza afisa mtendaji wa kata ya Ikuna bwana Job Fute baada ya kuhamishwa toka kata ya Igwachanya.
Hapa ndipo mkutano ulipo anzia kabla mvua kuanza kunyesha.
Uongozi wa kijiji hicho na kata kulia ni Afisa mtendaji wa kata bwana Job Fute akifuatiwa na Diwani wa kata hiyo ya Ikuna bwana Valentino Hongoli kulia kwake akiwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Matiganjola bwana Razalo Mwinami akifuatiwa na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho bwana Samson Nyagawa.
Wananchi wa kijiji cha Matiganjola wilayani Njombe wakiingia ukumbini kwa kukimbia mvua
Vijana katika kijiji cha matiganjola wakiendelea na mchezo wa Pooltable,moja ya michezo iliyopigwa marufuku kuchezwa nyakati za asubuhi.
Hapa ni baada ya kukimbia mvua na kuhamia ndani ya ukumbi wa kijiji hicho.
Pamoja na mvua kuendelea kunyesha laki ni wananchi hao hawakuwa tayari kuondoka katika mkutano huo wakisiliza kupitia madirishani.
Afisa mtendaji wa kata ya Ikuna wilayani Njombe bwana Jobu Fute amepiga marufuku wafanyabiashara wa pombe kuuza pombe hizo majira ya asubuhi kinyume na sheria.
Kauli hiyo ameitoa jana katika kijiji cha matiganjola wakati wa mkutano wa hadhara wa kusoma taarifa ya mapato na matumizi ya kipindi cha miezi mitatu kijijini humo.
Bwana Fute amesema kuwa mfanyabiashara yeyote atakaye kutwa anauza pombe majira ya asubuhi atapigwa faini ya shilingi laki moja na nusu huku mteja atakaye kutwa akinywa pombe mda huo naye atatozwa shilingi laki moja.
Aidha mtendaji huyo amewataka viongozi wa vijiji vya kata hiyo kuwa mstari wa mbele katika uchangiaji wa michango ya ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Ikuna hatimaye wananchi nao wachangie.
Ameongeza kuwa ni marufuku kuona vijana wanashinda wanacheza pooltable na kamali usiku kucha ikiwa kuna shughuli kibao za kimaendeleo.
Amewataka wananchi kuongeza bidii katika michango hiyo kutokana na kiwango kuwa duni kulingana na hali ya fedha iliyopatikana ikiwa hadi sasa zimepatikana zaidi ya shilingi milioni Nne tu kati ya shilingi milioni 13 zinazohitajika.
Akisoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sasa afisa mtendaji wa kijiji hicho cha Matiganjola bwana Samson Nyagawa amesema kuwa hadi kufikia jumla kuu ya fedha iliyopo ni zaidi ya shilingi milioni tisa.
Valentino Hongoli ni diwani wa kata ya Ikuna ambaye amewataka wananchi kutumia muda huu vizuri kwa kuwapeleka watoto wao shule kwani hadi sasa ni kiasi kidogo cha wanafunzi walioripo katika shule ya sekondari Ikuna kwa kidato cha kwanza.
Wakati ukimalizika mkutano huo uliojaza mamia ya wakazi wa Ikuna licha ya kuwepo kwa mvua zilizopelekea kuhama eneo la mkutano na kuingia ukumbini lakini mwishoni likatolewa tamko na afisa mtendaji wa kijiji hicho kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliokaidi kushiriki mkutano huo wanatakiwa kulipa bati mojamoja
No comments:
Post a Comment