Wananchi wanamtoa marehemu kutoka kwenye chumba alichojinyongea kwenda kuyalaza chumba kingine nyumbani hapo.
Wananchi wanaingia katika chumba cha jikoni alikojinyongea marehemu kuchukua mwili wake kuhamishia chumba kingine.
Mkazi wa Mtaa wa Mgendela Edward Msigwa Ambaye Aliyekuwa Dereva Taxi Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Amekutwa Amefariki Baada ya Kujinyonga Kwa Kutumia Kamba ya Manira Kwenye Jiko la Nyumba Yake.
Wakiongea na Kituo Hiki Eneo la Tukio Mashuhuda wa Tukio Hilo Wamesema Tukio Hilo Limetokea Jana Majira ya Saa Nane Mchana na Kwamba Hakuacha Ujumbe Wowote.
Katika Tukio Jingine Mtoto Anayekadiliwa Kuwa na Umri wa Siku Moja
Amekutwa Amefariki Kwenye Mtaro wa Maji Machafu Eneo la Kilimahewa Mtaa wa Mwembetogwa Mjini Makambako Baada ya Kutelekezwa na Mama Yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Matukio Hayo na Kusema Kuwa Mtoto Huyo Ameokotwa Majira ya Saa Tatu na Nusu Asubuhi na Mwili wa Mtoto Huyo Umehifadhiwa Katika Zahanati ya Makambako.
Kamanda Ngonyani Amesema Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Juu ya Matukio Yote Mawili Ikiwa ni Pamoja na Kumtafuta Mama Aliyemtupa Mtoto Huyo Ambapo Ametoa Wito Kwa Wananchi Kutoa Taarifa Zitakazofanikisha Kukamatwa Kwa Mama Huyo.
No comments:
Post a Comment