Vijana wakionyesha kaburi ambalo mzoga huo wa ng'ombe ulizikwa likiwa na mabaki ya nyama |
Haya ni mabaki ya mzoga huu baada ya kuzikwa tena leo |
TABIA ya baadhi ya wakazi wa mkoa wa Iringa kupenda nyama nyama
bila kuangalia ni wapi wanakula ama kununua nyama hiyo ,imewatokea
puani wakazi wa Ikonongo kata ya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa
baada ya kuuziwa nyama ya mzoga wa ng'ombe aliyekufa kwa sumu toka
usiku wa jana.
Wananchi hao wamejikuta katika majuto baada ya kujisikia dalilia za
matumbo kuuna baada ya kufakamia nyama hiyo ya mzoga kwa zaidi ya
siku mbili sasa.
wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com leo
baadhi ya wafanyakazi wa shamba la mifugo la raia wa nchini China
ambao walishuhudia kifo cha ng'ombe huyo na kuzikwa kwake ,walisema
kuwa ng'ombe huyo alikufa toka jana na kuzikwa baada ya kuchukuliwa
vipimo na kuonekana kifo chake kimesababishwa na sumu .
Bila kutaja aina ya sumu iliyopelekea kifo cha ng'ombe huyo walidai
kuwa baada ya kupimwa lilichimbwa shimo kubwa na kufukia mzoga
huyo huku mwenzao huyo akionyesha tamaa kwa kuwaomba wasifukie sana
mzoga huyo.
Hata hivyo baada ya kukamilisha zoezi la kufukia mzoga huyo
inadaiwa kuwa mwenzao mmoja aliyefahamika kwa jina la Abdu alirudi
usiku na kufukua mzoga huyo na kumchunja ngozi kisha kupeleka kijiji
kufungua bucha la nyama na wananchi wa eneo hilo kuchangmkia
kununua nyama hiyo ya bei ya kutupwa .
Salome kalinga ni mmoja kati ya wakazi wa Ikonongo ambae alipata
kula nyama hiyo amesema kuwa bei ya kutupwa ambayo nyama hiyo
ilikuwa ikiuzwa ndio iliwasukuma wananchi wengi kuchangamkia nyama
hiyo na hata kununua ya kutosha kwa kwenda kuweka akiba majumbani
kwao.
"Sisi tuliambiwa kuwa mchina huyo ameamua kutoa sadaka kwa wakazi hao
kwa kumkubali kuwa muwekezaji katika eneo hilo hivyo kilo la nyama
badala ya kuuzwa shilingi 5000 kama ilivyo buchani kijana huyo
alikuwa akiuza shilingi 2000 hadi 1000 na iwapo unapungufu unaongea"
Alisema kuwa baada ya kula nyama hiyo kwa siku mbili mfululizo sasa
ndipo leo wamebaini kuwa nyama hiyo si nyama tena bali ni mzoga na
hivyo kuamua kufanya msako na kufanikiwa kuwakamata wauzaji wawili
akiwemo kijana huyo ambae baadae alitoweka.
Hivyo hadi sasa kijana mmoja amekamatwa akiwa na nyama kilo 10
ambazo alikuwa akiendelea kuuza na kupewa kichapo kabla ya kupelekwa
polisi.
Tabia ya wananchi wa Iringa kuchangamkia mishkaki na nyama ambayo
inauzwa kwa bei ya kutupwa imeendelea kukua na hivyo ili kuepuka
kulishwa mizoga ni vema tahadhari zaidi kuchukuliwa na walaji nyama.
No comments:
Post a Comment