Rais
wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati,
Matanzania Onesmo Ngowi atasimamia pambano la ubingwa wa dunia la
vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini.
Mpambano huo utawakutanisha mabondia Ilunga Makaba kutoka Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) mwenye makazi yake nchini Afrika ya Kusini akipambana na bondia Gogita Gorgiladze
anayetoka katika jiji la Tiblis, nchini Georgia. Georgia ilikuwa kati
ya nchi zilizokuwa Umoja wa nchi za Kisoshalisti wa Sovieti (USSR).
Mabondia
hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12)
watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa dunia (Youth Title) wa
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight
tarehe 15 February, 2013.
Mpambano
wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace
in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South
Africa.
Ngowi kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba moja:Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar (Spain) na Jaji namba tatu: Jaap Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini).
Mpambano
huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha
mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa “Utali wa Michezo”
Imetolewa na:
UTAWALA
IBF/ AFRIKA
International Boxing Federation Africa (IBF/AFRICA)
Benjamin William MkapaPension Towers
Mezzanine Floor, AzikiweStreet
Dar-Es-Salaam - Tanzania
Dar-Es-Salaam - Tanzania
Technology House, 35-38Ghalla Road,
P.O BOX 1106, Moshi -Tanzania
Cell: 255-754-360828
E-mail: ibfafrica@yahoo.com
No comments:
Post a Comment