mwenyekiti mteule wa IPC Frank Leonard (kushoto) na katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin kulia tukiteta jambo katika moja kati ya vikao vyetu mwaka jana |
Aliyekuwa mweka hazina wa IPC marehemu Vicky Macha |
Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Marehemu Daud Mwangosi na chini siku alipouwawa kinyama |
katika uchaguzi huo uliofanyika leo wakati wa mkutano maalum wa uchaguzi wa IPC uliofanyika Hotel ya M.R mjini Iringa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Frederick Siwale aliwataja waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard aliyepata kura 17 kati ya kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti iliyokuwa ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza kujitoa na kuomba wajumbe kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri , wakati makamu mwenyekiti amepita bila kupingwa Jackson Manga aliyepata kura zote 18 za wajumbe wa mkutano huo ambao jumla ya wanachama hai wa IPC ni 24 ila waliofika leo ni 18 wakati nafasi ya katibu mtendaji wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin aliyepata kura za ndio 16 huku kura 2 zikimkataa .
Wengine waliochaguliwa ni pamoja na mweka hazina mkuu wa IPC Janeth Matondo aliyechukua nafasi ya marehemu Vicky Macha kwa kupata kura zote za ndio 18 pamoja na mweka hazina msaidizi Suleiman Boki aliyepata kura zote 18 .
Wajumbe watatu waliochaguliwa ni Hapy Matanji aliyepata kura (18) Swiga Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).Imetoka kwa Mdau wa matukio Francis Godwin Iringa.
No comments:
Post a Comment