MLEZI
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) na
mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Salim Abri (Asas) achangisha
kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 7.4 huku mwenyewe akiwachangia
wanahabari Iringa kiasi cha Milioni 2 taslimu katika harambee ya
kuchangia asasi ya kuweka na kukopa ya
wanahabari wa mkoa wa Iringa (IPC Vicoba).
Pamoja na Asas pia mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) alichangia kiasi cha shilingi 500,000 taslimu wakati mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao ( CHADEMA) akichangia mchango wa shilingi 150,000 akiwa wodini anakoendelea kutibiwa,wakati mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiahidi kuchangia kiasi cha shilingi 200,000,mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi akichangia taslim kiasi cha shilingi 100,000
.
Pamoja na Asas pia mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) alichangia kiasi cha shilingi 500,000 taslimu wakati mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao ( CHADEMA) akichangia mchango wa shilingi 150,000 akiwa wodini anakoendelea kutibiwa,wakati mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiahidi kuchangia kiasi cha shilingi 200,000,mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi akichangia taslim kiasi cha shilingi 100,000
.
Katika
harambee
hiyo iliyofanyika jana kwenye Mkutano Mkuu wa Wadau wa Habari
uliofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa blog ya Francis
Godwin iliahidi kuchangia kiasi cha shilingi 200,000 Blog ya Mjengwa
aliahidi 100,000
wakati mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi akichangia shilingi
300,000 pamoja na benki ya wananchi Mufindi ambayo pia iliahidi
kuchangia kiasi cha shilingi 300,000.
Wengine
waliochanga katika harambeee hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa Jesca Msambatavangu Sh 200,000, Mkuu wa Wilaya Kilolo, Gerald Guninita
Sh 200,000 ,na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM) Rita Kabati
(CCM) Sh 100,000.
Jeshi
la Polisi waliahidi kuchangia Sh 300,000, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine
Ishengoma Sh 100,000 Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya GNMS Geofrey Mungai Sh
150,000 na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk Leticia Warioba Sh 100,000.
Aidha baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) liliahidi shilingi 100,000,UVCCM Iringa vijijini 100,000,Mwakilishi wa Habari leo Iringa (100,000),IMTV(100,000)Country Fm (100,000),Nuru Fm ( 70,000), Ebony Fm (80,000),Qbla Ten (50,000), Furaha Fm(50,000),ICISO (100,000) madiwani Manispaa ya Iringa (250,000) na wengine wengi.
Wengine
akiwemo Mhifadhi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa), vyombo vya
habari vya mkoani na wadau mbalimbali walichanga kati ya Sh 50,000 na Sh
100,000 huku wanahabari wenyewe wakichanga zaidi ya Sh Milioni 2.
Akishukuru
kwa michango hiyo, Mwenyekiti wa IPC Vicoba Janeth Matondo aliwashukuru wadau
wa habari mkoani hapa kwa kukisaidia chama hicho kupata mtaji.
“Mtaji
huu utatumika kuboresha shughuli mbalimbali za kimaendeleo za wanahabari mkoani
hapa,” alisema.
Alisema
pamoja na kukopeshwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi, mikopo
mingine itakayotolewa italenga kuinua shughuli za kijasiriamali za wanahabari
wa mkoa wa Iringa.
Awali
Salim Abri ambaye pia ni mlezi wa Klabu ya Wanahabari Mkoa wa Iringa (IPC)
aliwapongeza wanahabari kwa kuanzisha chama hicho.
“Ndugu
zangu wadau, wanahabari ni watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la
maendeleo ya taifa, lakini wengi wao hawajaajiriwa, wanafanya kazi kwa malipo
haba, kwahiyo chombo hiki kitasaidia kubadili maisha yao,” alisema na kuwasihi
wadau walioahidi kutoa michango kutimiza ahadi zao.
Aliutaka
uongozi wa IPC kufuatilia michango iliyoahidiwa na kuomba michango zaidi kutoka
kwa wadau wengine ili kukiimarisha chombo hicho.
Wakati katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard alisema kuwa lengo la kuanzisha IPC VIKOBA ni kutaka wanahabari mkoa wa Iringa kujitegemea na kutumia chombo hicho kukopa kwa ajili ya kujenga nyumba ama kununua vitendea kazi .
MWISHO.Imetoka kwa mdau wa matukio Francis Godwin Iringa.
No comments:
Post a Comment