Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
#BMGHabari
Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Mgeni
Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro,
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye
uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania,
uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Afisa
Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua
ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo
kitaifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
George Binagi-GB Pazzo
Wakazi
wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini,
wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua
kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya Sun King.
Meneja
Masoko wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii
leo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King
ambazo ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.
“Kila
Kijiji nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao
watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia
mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni
Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo
taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.
Mkuu
wa Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo
imedhamiria kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya
umeme pamoja na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei
nafuu.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za
King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana,
amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani
kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira
zaidi kwa vijana. Tazama hapa uzinduzi zaidi
No comments:
Post a Comment