KIKOSI KAZI KILICHOUNDWA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KWAAJILI YA KUSHUGHULIKIA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI VINAVYOTIRIRISHA MAJI YAKE KUELEKEA MTO RUAHA MKUU
MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE MOHAMED ALLY KASINGE AKIZUNGUMZA MBELE YA KIKOSI KAZI HICHO AKIWA KATIKA UKUMBI WA WILAYA YA WANGING'OBE
MWENYEKITI WA KIKOSI KAZI KILICHOUNDWA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMBAYE PIA NI KATIBU TAWA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU AKITOA MAELEKEZO
Diwani Wa Kata Ya Ulembwe Agnetha Mpangile akichangia Hoja
Katibu Tawala Wilaya Ya Wanging'ombe
mkurugenzi wa Wilaya Ya Wanging'ombe Amina Kiwanuka Akizungumza Mbele Ya Kikosi Kazi Hicho Cha Mazingira
WANGING'OMBE
Kikosi Kazi Kilichoundwa Na Makamu Wa Rais Samia Suluhu Kwaajili Ya Kusimamia Utunzaji Wa Mazingira Na Vyanzo Vya Maji Kimehimiza Wananchi Na Viongozi Kushikamana Kutunza Mazingira Kwa Kupanda Miti Ambayo Ni Rafiki Na Vyanzo Vya Maji Kwa Faida Ya Sasa Na Baadaye.
Hayo Yamesemwa Na Mwenyekiti Wa Kikosi Kazi Cha Utunzaji Mazingira Na Vyanzo Vya Maji Mkoa Wa Njombe Na Mbeya Ambaye Ni Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Jackson Saitabahu Wakati Wa Majumuisho Ya Ziara Yake Ya Siku Mbili Ya Kutembelea Vyanzo Vya Maji Vinavyotiririsha Maji Kuelekea Mto Wa Ruaha Mkuu.
Saitabahu Amesema Kuwa Swala La Vinyungu Linatakiwa Kutiliwa Mkazo Kwa Kutoruhusu Wakulima Kurudi Mabondeni Kuendelea Na Kilimo Hicho Kwenye Vyanzo Vya Maji Na Kusema Kuwa Elimu Inatakiwa Kutolewa Kwa Wingi Juu Ya Sheria Za Utunzaji Wa Mazingira Na Vyanzo Vya Maji.
Kwa Upande Wake Mkuu Wa Wilaya Ya Wanging'ombe Mohamed Ally Kasinge Ameahidi Kuunda Kikosi Kazi Cha Kushughulikia Utunzaji Wa Mazingira Ambayo Mwenyekiti Wake Atakuwa Yeye Mwenyewe Huku Akisema Yale Maagizo Yanayohitaji Kufanyiwa Kazi Ndani Ya Muda Mfupi Yanatakiwa Kushughulikia Haraka Ikiwemo Kuondoa Miti Isiyo Rafiki Na Vyanzo Vya Maji.
Wenyeviti Wa Serikali Za Vijiji Vya Nyumbanitu,Mlevela Na Igima Wameshukuru Kwa Kutembelewa Na Kikosi Kazi Hicho Na Kusema Kuwa Wananchi Na Halmashauri Za Vijiji Bado Zinaendelea Na Juhudi Za Kutoa Elimu Ya Mazingira Kwa Wananchi Wote Ambapo Tayari Baadhi Ya Wananchi Wameanza Kuwa Uelewa Juu Ya Utunzaji Mazingira Na Kuanza Kupanda Miti Rafiki Na Vyanzo Vya Maji.
Timu Ya Kikosi Kazi Kilichoundwa Na Makamu Wa Rais Kushughulikia Mazingira Kimefanikiwa Kutembelea Vyanzo Vya Viwili Vya Maji Mbukwa Na Mto Mtitafu Ambayo Inatiririsha Maji Kuelekea Mto Wa Ruaha Mkuu Na Kufanikiwa Kuzungumza Na Viongozi Mbalimbali Wa Vyama Na Serikali .
No comments:
Post a Comment