Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya,Mh Amos Makalla ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka mkoa
wa Songwe mapema jana,jijini humo huku vifijo na nderemo za kuwasili
mwenge huo vikiwa vimeshamiri,Hafla ya kuupokea Mwenge huo imefanyika
Wilayani Chunya April 16,2017.Mwenge huo ukiwa mkoani Mbeya utakimbizwa
katika halmashauri saba,ambapo utafanya kazi ya kukagua,kuzindua na
kuweka Mawe ya Msingi miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi
Bilioni 10.8
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akiupokea Mwenge wa Uhuru wilayani
Chunya mkoani Mbeya sambamba na kula kiapo cha kuukimbiza mwenge huo
katika halmashauri zote za mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya makamanda wa jeshi la Polisi ambao pia ni miongoni Mwa wakimbiza mwenge wa Uhuru uliowasali hapo mkoani Mbeya
No comments:
Post a Comment