Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa
niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa sista Stella Selugenge wa Kituo cha Kulelea watoto cha Msimbazi
Center leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa
niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa Afisa Ustawi wa Jamii wa Mahabusu ya Taifa ya watoto Upanga Bi
Isabella Shitindi leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa
niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa Bibi Sherry Mavura Mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha SOS
Children village Cha Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Bw. Rabikira Mushi akikabidhi zawadi za Pasaka kwa
niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa Bibi Veronika Msanjila wa Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge
leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
Na Anthony Ishengoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa
zawadi zenye thamani ya Shilingi milioni 11,782,000/= kwa jumla ya vituo 9
katika Mkoa wa Dar es Salaam, 2 Zanzibar na 21 kutoka kwenye mikoa ya
Tanzania Bara kwa ajili sikukuu ya Pasaka .
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mhe. Rais,Kamishna wa Ustawi wa jamii
Bw. Rabikira Mushi amesema utoaji wa zawadi hizi umekuwa ni utaratibu wa
kawaida kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kutoa zawadi za vyakula
kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha makundi yenye
mahitaji maalum kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu
wengine.
Akifafanua Mushi amesema Mikoa ingine iliyofaidika na zawadi hizo ni
Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Shinyanga, Morogoro, Kigoma, Ruvuma,
Mara, Kagera, Manyara, Tabora, Lindi Mtwara, Singida, Mwanza, na Pwani.
Aidha vitu vilivyofaidika na zawaidi hizo kwa mkoa wa Dar es Salaam na
Zanzibar ni,Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Makao ya Watoto
Mburahati,Makao ya Watoto Msimbazi.Makao ya Watoto Kijiji cha
Furaha,Makao ya Watoto SOS Children’s Village Tanzania.
Viuo vingine ni Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund, Temeke.Makao ya
Watoto Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization),Mahabusu ya
Watoto Dar es Salaam, Upanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza na wenye
Ulemavu Nunge Kigamboni.
Kwa upande wa Zanzibar Bw. Mushi alitaja Vituo vilivyonufaika na zawadi
hizo,Kituo cha Watoto Istima - Chakechake, PembaMakazi ya Wazee
Wasiojiweza Sebleni – Unguja.
Aidha kwa Mikoa ya Tanzania Bara jumla ya vituo 21 vimefaidika na zawadi ya
Mhe. Rais na baadhi yake ni Mahabusu ya Watoto Moshi,Makazi ya Wazee
Wasiojiweza Njoro – Kilimanjaro,Mahabusu ya Watoto Mbeya,Mahabusu ya
Watoto Arusha,Mahabusu ya Watoto Tanga,Makao ya Wazee Wasiojiweza
Mwanzage Tanga,Makazi ya Wazee Wasiojiweza Misufini Tanga.
Utoaji wa zawadi umekuwa ni utaratibu wa kawaida wa Waheshimiwa Marais
tangu awamu ya kwanza makundi haya maalum yamekuwa yakipatiwa zawadi
za vyakula kama vile mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ili kuwawezesha
kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment