ERASTO MKIWA MRATIBU WA MIRADI KATIKA SHIRIKA LA PAD AKISOMA TAARIFA MBELE YA MGENI RASMI
WASHIRIKI WA KUTOKA HALMSHAURI ZA MKOA WA NJOMBE WAKIWA KWENYE SEMINA HIYO
MSAADA WA KOMPYUTA WAKIPEWA WASHIRIKI WA MAFUNZO HAYO
WANUFAIKA WAKIPEANA MKONO NA MGENI RASMI BAADA YA KUPOKEA MSAADA WA KOPYUTA
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PAD AKISHIRIKIANA KUFUNGUA KOPYUTA WOTE WAZIONE
MATISHETI YAKABIDHIWA KWA WASAIDIZI WA KISHERIA
SASA WASAIDIZI WA MSAADA WA KISHERIA WANAKWENDA KUPUNGUZA MIGOGORO MBALIMBALI KATIKA JAMII MKOA WA NJOMBE
KATIBU WA SHIRIKA LA UPENDO NYOMBO JOAKIM MWINAMI NAE AKIWA KWENYE MAFUNZO YA WASAIDIZI WA KISHERIA YALIOTOLEWA NA SHIRIKA LA PAD YALIOFANYIKIA UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO NJOMBE MJINI
MKURUGENZI SHIRIKA PAD ISKAKA MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NJOMBE
NJOMBE
Shirika Lisilo La Kiserikali La PADI Limekabidhi Kompyuta Mpakato Yaani Laptop 6 Kwa Wasaidizi Wa Msaada Wa Kisheria Wa Mkoa Wa Njombe Kwaajili Ya Kurahisisha Utekelezaji Wa Majukumu Na Kuandalia Taarifa Zinazohusu Sheria Ili Kuzisaidia Jamii Vijijini.
Akizungumza Mara Baada Ya Kukabidhi Kompyuta Hizo Zilizoandaliwa Na Shirika La PADI Afisa Maendeleo Ya Jamii Mkoa Wa Njombe Bwana William Waziri Ametaka Wasaidizi Hao Kuzitumia Kwa Umakini Pasipo Kuzipoteza Na Kuharibu Pamoja Na Kuzitumia Kwa Malengo Ya Kusaidia Jamii.
Bwana Waziri Amesema Kompyuta Hizo Zitumike Kuhifadhi Na Kuwahisha Taarifa Pale Zinapotakiwa Na Kuondoa Uzembe Katika Utumaji Wa Taarifa Kwa Wakati Na Kuwataka Kwenda Kufanya Kazi Za Kusaidia Wananchi Katika Kutatua Matatizo Yanayohusu Migogoro Na Marumbano Yanayoweza Kusababisha Madhara.
Akizungumza Na Uplands Fm Mkurugenzi Wa Shirika La PAD Iskaka Msigwa Amesema Kuwa Shirika Hilo Lina Lengo La Kuondoa Umasikini Kwa Watanzania Kwa Kutetea Haki Mbalimbali Zikiwemo Wazee Kupewa Penshen Ya Uzeeni Na Kushawishi Watunga Sera Kurekebisha Sera Zisizo Rafiki Kwa Wachache Na Kusaidia Jamii Kujua Haki Zao Kwa Kupewa Msaada Wa Kisheria.
Kwa Upande Wake Washiriki Wa Semina Hiyo Iliyolenga Kutoa Elimu Kwa Wasaidizi Wa Msaada Wa Kisheria Wa Kutoka Halmashauri Sita Za Mkoa Wa Njombe Wamesema Kuwa Mafunzo Waliyoyapata Yatasaidia Kuandika Maandiko Mbalimbali Ya Kuombea Misaada Kwa Wafadhili Na Kushiriki Kikamilifu Kutatua Migogoro Iliyo Mingi Inayotawala Kwenye Maeneo Yao.
Afisa Miradi Wa Shirika La PAD Erasto Mkiwa Amesema Wamelazimika Kutoa Mafunzo Kwa Wasaidizi Wa Msaada Wa Kisheria Ili Wakawasaidie Wasiyo Na Uwezo Wa Kufahamu Sheria Ambapo Wshiriki Wa Semina Hiyo Watakuwa Na Jukumu Kubwa La Kutetea Haki Za Wanyonge Waliopo Kwenye Maeneo Yao.
No comments:
Post a Comment