MBUNGE WA LUPEMBE JORAMU HONGORI AKIJADILIANA JAMBO NA AFISA TARAFA BWAANA MWELANGE WAKIWA KICHIWA
WANANCHI WA KATA YA KICHIWA WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA WAKIMSIKILIZA MBUNGE WA LUPEMBE
MBUNGE WA LUPEMBE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IKANDO KATA YA KICHIWA
MBUNGE JORAM HONGORI AKIWA KATIKA KIJIJI CHA IBUMILA KWENYE MKUTANO WA HADHARA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAKE
WAKANDARASI WALIOKWENDA KUTOA ELIMU YA KUINGIZIWA UMEME KWA KUSUKIWA WAYARING KWENYE NYUMBA ZA WANANCHI
MBUNGE JORAMU HONGORI AKIZUNGUMZA JAMBO NA AFISA TARAFA YA MAKAMBAKO MWELANGE
DIWANI WA KATA YA KICHIWA PETER NYAHUYA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
MBUNGE ALIPOTEMBELEA KATIKA KITUO CHA AFYA KICHIWA NA HAPA AMEKUTANA NA MGANGA MFAWIDHI WA KITUO CHA AFYA KICHIWA
NJOMBE
Baadhi Ya Viongozi Wa Serikali Za Vijiji Vya Kata Ya Kichiwa Wilayani Njombe Wakiwemo Wenyeviti Wametuhumiwa Kushiriki Kuwanyang'anya Haki Akina Mama Wajane Ambapo Wamedaiwa Kuwanyang'anya Mashamba Na Miti Kwa Kuwasimamia Wenye Uwezo.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Wananchi Wa Kijiji Cha Ibumila Mbele Ya Mbunge Joram Hongori Ambapo Wametoa Kilio Chao Cha Kudhurumiwa Mali Na Maeneo Ya Mshamba Huku Wenyeviti Wa Serikali Za Vijiji Hivyo Wakishindwa Kuwasikiliza wanaopolwa Maeneo Yao Kwa Kuegemea Kwa Wapolaji.
Katika Hatua Nyingine Wananchi Hao Hususani Akina Mama Wajane Wamesema Wamekuwa Wakinyimwa Haki Zao Hata Za Kumiliki Mali Katika Ukoo Ambapo Wamemuomba Mbunge Huyo Kuhakikisha Anahimiza Serikali Kupeleka Wanasheria Wa Msaada Wa Kisheria Kutetea Haki Zao.
Kwa Upande Wake Mbunge Wa Lupembe Joramu Hongori Amesema Serikali Imetunga Sheria Ya Kuwasaidia Wananchi Katika Kutatua Migogoro Na Kulinda Haki Kwa Kila Mmoja Katika Jamii Kwa Kupitisha Sheria Ya Kuwepo Kwa Wasaidizi Wa Kisheria Kwenye Maeneo Mbalimbali Ya Vijiji.
Bwana Hongori Amesema Wasaidizi Wa Msaada Wa Kisheria Watasaidia Kuwatetea Wanyonge Ambao Wamekuwa Wakidhurumiwa Haki Zao Na Wenye Uwezo Wa Kifedha Na Ufahamu Wa Sheria Wanaohusika Kunyang'anya Haki Kwa Kutumia Vyombo Vya Sheria Kwa Kutengeneza Uongo Kuwa Ukweli.
Kwa Upande Wake Baadhi Ya Wenyeviti Wa Vijiji Vya Kata Ya Kichiwa Vikiwemo Vya Ibumila,Maduma Na Kichiwa Wamekanusha Kuwepo Kwa Tatizo Hilo Na Kusema Kuwa Kama Lipo Labda Litakuwepo Kwa Vijiji Vingine Huku Wakiahidi Kulifuatilia Kwa Kiina.
No comments:
Post a Comment