Saturday, February 25, 2017
ZAIDI YA WATOTO 200 WAPATA UBATIZO NA EKARIST YA KWANZA KANISA KATHOLIKI NJOMBE
NJOMBE
Wazazi Na Walezi Wa Kanisa Ktholiki Jimbo La Njombe Wameombwa Kuwalinda Watoto Ambao Wamepatiwa Ubatizo Na Sakaramenti Ya Ekaristi Takatifu Na Kuwapatia Elimu Ya Maadili Ya Kiroho Kwaajili Ya Kulitumikia Taifa La Wakristo Nchini.
Rai Hiyo Imetolewa Na Paroko wa Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Padre Francisco Chengula Wakati Akitoa Enjili Kwa Waumini Wa Kanisa Hilo Katika Sherehe Ya Ubatizo Na Kuwapatia Ekarist Takatifu Yaani Comunyo Ya Kwanza Kwa Watoto.
Pd.Chengula Amesema Wasimamizi Wa Watoto Waliopewa Ubatizo Na Ekarist Takatifu Wanapaswa Kuwalinda Na Kuhimiza Kila Siku Kwenda Ibadani Katika Jumuiya Ndogondogo Na Kanisani Na Kufuatilia Myenendo Yao Kama Inampendeza Mungu.
Pd.Chengula Amesema Kuwa Wazazi Na Wasimamizi Wa Watoto Wanatakiwa Kutafuta Mbinu Za Kila Aina Kuhakikisha Watoto Waliopo Ndani Ya Ukrsito Wanakwepa Vishawishi Vya Aina Yoyote Ambavyo Vinaweza Kuwasababishia Madhara Kwa Kuacha Tamaa Zisizo Na Faida.
Hata Hivyo Chengula Amewaasa Watoto Kuwa Wadilifu Wakati Wa Mafundisho Na Kuwaheshimu Wazazi,Kuacha Tamaa Za Kimwili, Wizi ,Urafi Na Anasa Mbalimbali Ambazo Hazimpendezi Mungu Huku Akitaka Kutambua Jukumu Lao Kubwa La Kusali Na Kusoma Kwa Bidii Kwa Manufaa Yao.
Pd. Chengula Ametoa Huduma Ya Ubatizo Na Ekarist Takatifu Yaani Komunyo Ya Kwanza Katika Kanisa Katholiki Jimbo La Njombe Kwa Watoto 2015 Kwenye Sherehe Za Ubatizo Na Ekaristi Takatifu Iliyofanyika Kanisani Hapo.
Kwa Upande Wake Padre Laurent Mwalongo Wa Parokia Ya Sonji Akizungumza Mara Baada Ya Kukamilika Kwa Misa Ya Ubatizo Na Ekarist Takatifu Jimboni Hapo Amewashukuru Wazazi Na Walezi Kwa Mshikamano Mkubwa Waliouonesha Kwa Watoto Na Kuahidi Kuendelea Kushirikiana Na Wazazi Katika Kuwalea Watoto Katika Malezi Ya Kikatoliki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment