MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIFYEKA NYASI MJINI MAKAMBAKO SIKU YA JUMA MOSI YA MWISHO WA MWEZI YA MWEZI FEBRUARY
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BAADA YA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA AKAELEKEA KUPANDA MTI MMOJA KATIKA VIBANDA VINAVYOZUNGUKA KITUO KIKUU CHA MABASI MAKAMBAKO KAMA UNAVYOMUONA HAPA.
WA PILI MWENYE KILEMBA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIELEKEA ENEO LA KUFANYIA USAFI KUZUNGUKA KITUO KIKUU CHA MABASI MJINI MAKAMBAKO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIPEANA MAELEKEZO NA WANANCHI WA MAKAMBAKO WAKATI WA KUFANYA USAFI KWAMBA HILI NI ENEO LA MTARO WA MAJI NYUMBA ZILIZOJENGWA MBELE ZINATAKIWA KUBOMOLEWA KIPANDE KIDOGO KWAAJILI YA KUPITISHA MTARO WA MAJI ULIOTOKA BARABARA KUU YA NJOMBE IRINGA
HUU NDIYO MTARO UNAOJADILIWA KWAMBA HALMASHAURI INATAKIWA KUJENGA KUPITIA KWENYE NYUMBA ZINAZOONEKANA MBELE HAPO
WANANCHI MAKAMBAKO NAO WAKIWA KWENYE SHUGHULI HIYO YA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA
HUU NI MOTARO UNAOTAKIWA KUJENGWA ILI MAJI YATOKE HAPA KUPITIA KWENYE NYUMBA ZILIZOPO MBELE YA MTARO HUU
MTARO WA MAJI UNAFANYIWA USAFI NA WANANCHI MAKAMBAKO
NJOMBE
Wananchi Wa Mji Wa Makambako Wilayani Njombe Wametakiwa Kujenga Mazoea Ya Kufanya Usafi Kila Mara Katika Maeneo Yao Bila Kusukumwa Na Viongozi Ambapo Kwa Atakutwa Mazingira Yake Yakiwa Machafu Hatua Kali Za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Luth Msafiri Wakati Akizungumza Na Wananchi Wa Mji Wa Makambako Mara Baada Ya Kushiriki Zoezi La Kufanya Usafi Wa Mazingira Katika Eneo Linalokizunguka Kituo Kikuu cha Mabasi Cha Makambako Ambapo Hapa Hakufrahishwa Na Watu Kujisaidia Haja Ndogo na Kubwa Kiholela.
Bi. Msafiri Amesema Kuwa Hatakuwa Tayari Kuona Mazingira Ambayo Ameshiriki Kufanya Usafi Katika Jumamosi Ya Mwisho Wa Mwezi Yanakuwa Machafu Kama Ilivyokuwa Hapo Awali Ikiwa Kuna Watu Wanafanya Biashara Kuzunguka Maeneo Hayo Lakini Wanasubiri Kusukumwa Na Viongozi .
Katika Hatua Nyingine Bi. Msafiri Amewahimiza Wananchi Wilaya Ya Njombe Kuendelea Kuthamini Uwepo Wa Miti Kwa Kuipanda , Kuitunza Na Kutaka Kila Mwananchi Kupanda Miti Isiyopungua Mitatu Kwenye Maeneo Yao.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Wa Mji Wa Mkambako Bwana Kazi Kuboma Amesema Zoezi La Kufanya Usafi Wa Mazingira Limepokelewa Vizuri Kwa Mji Wa Makambako Na Kusema Kuwa Maagizo Yaliotolewa Na Mkuu Wa Wilaya Halmashauri Hiyo Itakwenda kuyatekeleza ikiwemo Kujenga Mtaro Wa Maji Uliopo Na Kuchukua Hatua Kwa Vibanda Vinavyoendekeza Uchafu .
Mwenyekiti wa Kituo Kikuu cha Mabasi Cha Makambako Daniel Mwakasita Amesema Kuwa Swala La Kufanya Usafi Linatakiwa Kutekelezwa Na Kila Mmoja Pasipo Kusukumwa Na Kiongozi Ambapo Ameahidi Kutunza Mazingira Kuzunguka Kituo Kuhakikisha Yanakuwa Safi Muda Wote.
No comments:
Post a Comment