Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazi Umma wa
Watanzania kuwa Wizara imehamia rasmi Dodoma.
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga
Walio
keti ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katika), Naibu Katibu Mkuu Balozi
Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi
Rasilimali Watu Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa
katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara Mjini Dodoma
KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda
kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17
Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza
imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa
tarehe 17 Februari, 2017.
Miongoni
mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo
ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na
Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe.
Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao.
Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17
Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz
P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na
Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
Katika
Uhamisho huo wa Awamu ya Kwanza, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi
wao Wakuu.
Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa nikama ifuatavyo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.
Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi : +255-26-2323208,
Barua pepe : nje@nje.go.tz Tovuti : www.foreign.go.tz
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma, 27 Februari, 2017.
No comments:
Post a Comment