Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, January 21, 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIMU MAJALIWA IMEAHIRISHWA NJOMBE LEO


 
 WAZIRI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIMU MAJALIWA AKIWA KWENYE ZIARA MKOANI NJOMBE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
 

MKUUWA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA OFISINI KWAKWE KUHUSIANA NA KUAHIRISHWA KWA ZIARA YA MH.WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KASSIMU MAJALIWA KWAMBA AMEPATA DHARULA YA KISERIKALI ANATAKIWA KURUDI DAR ES SALAAM KUTEKELEZA MAJUKUMU HAYO NDIPO ATARUDI KUENDELEA NA ZIARA MKOANI NJOMBE. 


NJOMBE

Ziara ya Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa iliyokuwa ikiendelea Mkoani Njombe Kwa Siku  Sita  Imeahirishwa kutokana na Waziri huyo kuitwa Dar Es Salaamu Kwaajili ya Majukumu mengine ya kiserikali.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari Mkuu wa Wilaya ya Njombe Luth Msafiri amesema wananchi wa maeneo ambako ratiba ilikuwa inaonesha Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Atapita waendelee na majukumu mengine hadi hapo watakapo tangaziwa juu ya ujio wake tena.

Bi.Msafiri ametaka wananchi kuvuta subira wakati Waziri Huyo akiwa ameitwa Dar Salaamu kwaajili ya Kutekeleza majukumu ya Kiserikali ambayo ni lazima awepo bila kukosa ambapo amesema atakapo maliza majukumu hayo Dar Es Salaamu taarifa zitawafikia wananchi .

Amesema wananchi wawawie radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kutaka majukwaa waendelee kuyalinda ili atakapomaliza majukumu  Huko Dar Es Salaam atawajulisha wananchi juu ya kuendelea na ziara hiyo na wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi.

ziara  ya Waziri huyo imekuwepo kwa muda wa siku tatu Mkoani Njombe ambapo amefanikiwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya na kuzungumza na wananchi kuwaeleza dhamira ya serikali katika kutekeleza miradi hiyo .


No comments:

Post a Comment