Kaimu Meenja Uhusiano TANESCO, Bi.Leila Muhaji |
NA K-VIS BLOG.
SHIRIKA la Umeme
Tanzania (TANESCO) limesema, kwa sasa linafanya mabadiliko ya uongozi wa ndani
ya Shirika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Shirika kwa lengo la
kuongeza ufanisi zaidi na kazi hiyo ambayo tayari imeanza itakapokamilika, Umma
wa Watanzania utahafahimshwa kupitia vyombo vya habari.
Taarifa fupi iliyotolewa na
Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu TANESCO leo Januari 5, 2017 imeviomba vyombo vya
habari vitoe fursa fursa kwa Mamlaka husika kuendelea kukamilisha zoezi hili
muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla na taarifa rasmi itatolewa
baada ya zoezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment