PICHA YA PAMOJA NA WATOTO WALIOPO KITUO CHA TUMAINI WAKIWA NA KIKUNDI CHA AKINA MAMA WA KIKUNDI CHA HOPE VILLAGE BANK KILICHOPO ITUNDUMA KATA YA MTWANGO
HAPA NI KABLA HAWAJAINGIA KUWAONA WATOTO YATIMA
HAPA NDIYO WANAELEKEA KWA WATOTO HAO KUWAPATIA MSAADA WA MAHITAJI MBALIMBALI
KILA MMOJA AMETAMANI KUMBEBA MTOTO ALIYEMUONA KWENYE KITUO HICHO ILI KUWAFARIJI
WATOTO WAKUBWA NDIYO WANACHEZA NA KUWABEMBELEZA WALIOKO CHINI YAO
KATIKATI MWENYE NGUO TOFAUTI NA WENZAKE NI DIWANI WA VITI MAALUMU KATA YA MTWANGO BI.ROIDA WANDELAGE
KULIA MWENYE KILEMBA CHEUPE NI MLEZI WA WATOTO WA KITUONI HAPO SISTER DORATHEA MARIA AKIWA AMEONGOZANA NA AKINA MAMA WA KIKUNDI CHA HOPE VILLAGE BANK BAADA YA KUKABIDHI MSAADA KWA WATOTO
Na Michael Ngilangwa
NJOMBE
Kikundi cha akina mama wa kijiji cha Itunduma kata ya Mtwango Wilayani Njombe cha Hope Village Bank kimekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya nyumbani ukiwemo wa chumvi na sabuni kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Tumaini Ilunda.
Msaada huo uliotolewa na kikundi cha akina mama wa Kijiji cha Itunduma umegharimu zaidi ya shilingi laki mbili umetolewa na kikundi hicho baada ya kuchangishana wenyewe na kuomba msaada kwa wasamalia wema ambao wamechangia chochote walichokuwa nacho na hatimaye kupewa watoto hao.
Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya kikundi cha akina mama wa Itunduma cha Hope village Bank diwani wa viti maalumu kata ya Mtwango Roida Wandelage amesema kikundi hicho kinatoa mfano wa kuigwa kwa akina mama waliopo kata ya mtwango kwenda kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu waliopo kwenye kituo hicho.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa kikundi cha Hope Village Bank Joycy Mkanga amesema kikundi hicho kina wanakikundi 20 ambao wameanza tangu mwaka 2015 kukopeshana na wamefikia kupata kiasi cha shilingi milioni 11 ambapo kutokana na mafaniko wanayoyapata wamelazimika kuwachangia watoto hao.
Awali akizungumza mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi cha Tumaini kilichopo Ilunda Sister Dorothea Maria ameshukuru kwa msaada uliotolewa na kikundi hicho na wadau wengine ambapo muamko aumedaiwa kuwa mdogo kwa wazazi na walezi kwenda kuwasaidia watoto hao baada ya kuwaacha kituoni hapo.
Kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Tumaini Ilunda kina jumla ya watoto 85 ambao wanalelewa na kinachukuwa watoto ambao hawana wazazi wake wote na wale wenye mzazi mmoja ambaye hana uwezo wa kumlea mtoto wake na wale waliotelekezwa.
No comments:
Post a Comment