DKT MWAKYEMBE AKIZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA,WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WILAYA ZA MKOA WA NJOMBE NA IRINGA
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA HARISON MWAKYEMBE AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUKABIDHI TUZO NA CHETI KWA MIKOA YA NJOMBE NA IRINGA AKIWA CHUO CHA MAENDELEO CHA NJOMBE MJINI.
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA KUTOA SALAAMU
MKURUGENZI WA WILAYA YA WANGING'OMBE AMINA KIWANUKA BAADA YA KUPOKEA TUZO
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIPOKEA TUZO NA HATI YA KUONGOZA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI NA UTOAJI VYETI KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO
WAKUU WA WILAYA WAKIWA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE PAMOJA NA KATIBU TAWALA MKOA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUPOKEA TUZO YA MKOA
PICHA YA PAMOJA NA WASHIRIKI WALIOPOKEA TUZO HIYO WAKIWA NA MGENI RASMI WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT MWAKYEMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA OLE SENDEKA AKIWA NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA DKT HARISON MWAKYEMBE PAMOJA NA KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITABAHU
NJOMBE-Na Michael Ngilangwa Njombe-0757092504/06783217 72
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harison Mwakyembe amekabidhi Vyeti na Tuzo kwa Halmashauri na mikoa ya Njombe na Iringa ambayo imepata asilimia 98 ya kuongoza katika zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano bila malipo kwa nchi nzima ulioendeshwa chini ya Wakala wa Usajiri, Ufilisi na Udhamini RITA.
Waziri Mwakyembe amekabidhi Tuzo Hizo kwa Halmashauri za Mkoa wa Njombe Na Iringa baada ya kuongoza katika zoezi hilo la usajili wa vyeti vya kuzaliwa na kupongeza kwa hamasa iliyofanyika kwa mikoa hiyo ambayo miaka michache iliyopita maendeleo ya Usajili yalikuwa duni ambapo Njombe ilikuwa asilimia nane na sasa imefikia asilimia 98.
Waziri Mwakyembe amesema Mikoa ya Njombe Na Iringa imechangia kuijengea misingi imara ya maendeleo ya Nchi na kusema kuwa nchi yoyote ili ifanikiwe lazima iwe na takwimu sahahi za wakazi wake na kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kuanzisha Viwanda katika kuelekea Uchumi wa Kati wa Nchi ya Tanzania.
" Ili kutambua kazi kubwa mlioifanya ni vema tukakumbusha tulikotokea tulianza zoezi hili maalumu la uandikishaji watoto chini ya umri wa miaka mitano na kwamba vyeti bila malipo yoyote mwaka 2013 siyo kwamba tumeanza usajili mwaka 2013 tumeanza toka Uhuru ila tuliona kuna mkwamo mkubwa tukaona tuanzishe programu maalumu kuhakikisha na sisi tunaingia katika record kama wenzetu walioendelea kwa hiyo tukaanza hili zoezi Mkoani Mbeya ambako usajili ulikuwa asilimia 8.9 tu " Alisema Waziri huyo.
Waziri Mwakyembe amesema kufika mwaka 2015 Mkoa wa Mbeya ulikuwa umejikokota hadi kufikia asilimia 56 kwa kipindi cha miaka 3 Mkoa wa Songwe ulikuwa asilimia 8.9 kama Mbeya lakini mwaka jana walifikia asilimia 49 na programu ikahamia Mwanza ambapo Mwanza wao usajili ulikuwa kama asilimia 12. 1 mwaka jana wamefikisha asilimia 46 wakaamua kubadilisha Muundo wakahamia Mkoa wa Iringa na Njombe Ambako Kulikuwa na Asilimia 11.7 lakini kilichowashangaza ni kuona mikoa hiyo imefanya vizuri zaidi.
" Tulishangaa ,tulifrahi tukahamasika kwamba Mkoa wa Iringa ukatoka kwenye asilimia 11.7 hadi asilimia 95 ni mafanikio makubwa haijawahi kutokea na leo wanaongelea asilimia 100 ndani ya miezi mnne na kuvunja Record ya Dunia Na Njombe Ilikuwa asilimia 8.5 nayo ndani ya miezi mitatu na kufikia asilimia 98 kwa hiyo nawapa pongezi sana sana wana Njombe Na Iringa hadi Muwakilishi wa Unisef amesema mmevunja Record ya Dunia " Aliongeza Waziri Huyo.
Amesema Mikoa mingine ya Tanzania inapaswa kutembelea mikoa ya Njombe na Iringa Ili Kujifunza namna ilivyofanikiwa katika kutekeleza zoezi la kuhamasisha wananchi kupeleka watoto wao kuwasajili na kusema jitihada hizo ziendelee kufanyika hata kwa mikoa mingine kufikia asilimia walizopata mikoa ya Njombe na Iringa.
Akisoma taarifa Fupi mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Harison Mwakyembe ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa usajiri,Ufilisi na Udhamini RITA Bi. Emmy Hudson amesema Mkoa wa Njombe Na Iringa imeweza kuvuka malengo ya kusajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano mbapo RITA Imeamua kupongeza mikoa iliyofanya vizuri Ili kuwa mfano kwa Mikoa mingine.
Kwa Upande wake Wakuu wa Mikoa ya Njombe Na Iringa Christopha Ole Sendeka na Amina Masenza Wameshukuru kwa kupewa zawadi hizo na kusema mpango wa kusajili watoto ulianza mwezi Decemba 22 ,2016 zikitolewa kwenye ofisi za watendaji wa kata na vituo vya tiba za mama na mtoto nakwamba usajili huo sasa utakuwa ni agenda ya kudumu huku wakilishukuru shirika la Unisef kwa kuwa mdau katika zoezi hilo.
..............................................................................................................
No comments:
Post a Comment