Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri (Kushoto) akisalimiana na Maskauti kutoka Tanzania.
Skauti
27 kutoka shule mbili za msingi za Dar es Salaam wako nchini Kenya kwa
ziara ya wiki moja kwa mwaliko wa Chama cha Maskauti cha Kenya.
Watoto
hao kutoka shule za msingi za Canossa na Libermann, na maofisa wa Chama
cha Maskauti Tanzania waliowasindikiza, Kamishina Anthony Joachim na
Kamishina Saidi Debwani, leo wametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na
kusalimiana na Kaimu Balozi, Bi.Talha Mohamed Waziri.
Maskauti hao walimwambia Kaimu Balozi kuwa wametembelea maeneo mbalimbali ya Kenya na kujifunza mambo mengi.Kamishina Joachim amesema watoto hao wanatarajiwa kurejea nyumbani kesho.
Maskauti kutoka Tanzania na viongozi wao katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri.
No comments:
Post a Comment