Thursday, December 1, 2016
SHIRIKA LA HIGHLANDS HOPE UMBRELLA LA TUA ITULIKE NJOMBE
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA ITULIKE BWANA NG'ANDE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MTAA WAKE
WANANCHI WA MTAA WA ITULIKE WAKISIKILIZA KWA UMAKINI
MUKUFUNZI WA SHIRIKA LA HIGHLANDS HOPE UMBRELLA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI KUHUSIANA NA KERO ZINAZOIKABILI SEKTA YA AFYA KWA AKINA MAMA NA WATOTO KWENYE ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI
NJOMBE
Muuguzi wa zahanati ya Itulike Monica Mwakipesile amewataka wananchi wa mtaa huo kujiunga kwenye mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya CHF Kwaajili ya Kupatiwa matibabu kwa mwaka mzima unaoshirikisha watu sita katika familia moja.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa mtaa huo B.Mwakipesile amesema ili zahanati iweze kuwa na dawa za kutosha katika zahanati wananchi wanatakiwa kuchangia mfuko huo ambapo pesa hizo zitatumika kununulia dawa za kuwapatia wagonjwa wanaokwenda kutibiwa.
Bi.Mwakipesile amesema tatizo la kukosekana kwa dawa lililokuwepo hapo awali litakwenda kumalizika ambapo amesema ni watu 28 wa mtaa wa Itulike waliotekeleza zoezi la uchangiaji mfuko huo ikiwa mtaa unawatu wengi .
Kuhusu Huduma za matibabu bure kwa wazee Bi.Mwakipesile amesema zahanati hiyo haiwezi kuwapokea wazee wa aina yoyote ile watakaokwenda kupatiwa huduma za matibabu endapo watakuwa hawana vitamburisho vya kupatiwa matibabu bure ya wazee hao.
Baadhi ya wazee wa mtaa wa Itulike wamesema wapo tayari kutofika kwenye zahanati hiyo hata kama wamezidiwa kutokana na serikali kushindwa kutoa vitamburisho vya matibabu bure huku wananchi wakiwa na hofu juu ya kutoa shilingi elfu kumi kwaajili ya Bima ya afya kwa kile walichodai kukosa dawa kwenye zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Itulike Michael Ng'ande amewahakikishia wazee hao kwamba serikali itaendelea kufuatilia vitamburisho hivyo kutoka kwa viongozi wa halmashauri ili wapate huduma za matibabu kwenye zahanati hiyo.
Mkutano huo ambao umesimamiwa na shirika la Highlands Hope Umbrela unatarajia kuendelea katika mitaa mbalimbali ya kata za mjini Njombe lengo likiwa kupata changamoto ya afya inayowakabili akina mama na watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment