Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu
katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi
Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili
mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa
Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii
Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu
Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe
Christopher Olonyokie Ole-Sendeka.
Viongozi walioapishwa waki weka saini katika viapo vya maadili
Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi
Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na utalii Dkt.
Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu
Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher
Olonyokie Ole Sendeka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara
Alhaji Aliko Dangote akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es
Salaam. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki
wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji
cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji
cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA
IKULU
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana
na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo
hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya
Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika
kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema
kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara
hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi
huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote
kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya
kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.''Iwapo unataka
maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali
badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya
ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili '' amesema
Rais Magufuli.
Dokta Magufuli
amesema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu
ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni
watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake
mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote
ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu
amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema
hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
Katika
kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara
huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. Ameongeza
kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana
lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya
kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote
amemuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana
nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo
vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa
nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu
ya Tano.
Katika
hatua nyingine Rais Dkt.
John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Olonyokie
Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo
cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa
na Rais Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo
(Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa
Itifaki).
Jaffar
Haniu,
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es
Salaam.
10 Desemba,
2016.
No comments:
Post a Comment