Saturday, December 10, 2016
DC NJOMBE ATAKA HALMASHAURI YA MJI KUWAGAWIA VIJANA VIWANJA VYA KUJENGA NYUMBA ZAO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.LUTH ,MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI .
NJOMBE
Halmashauri ya mji wa Njombe Imetakiwa kuacha kugawa viwanja kwa upendeleo na kulifikilia kundi la vijana katika kusaidia kuwapatia viwanja hivyo kwaajili ya kujenga nyumba zao kuliko kugawa kwa wachache kama ilivyo kwa sasa.
Hayo yamesemwa na Vijana mjini Njombe mbele ya mkutano wa mkuu wa Wilaya ambapo wamepeleka malalamiko yao ya kushindwa kupewa viwanja na Halmashauri hiyo ambavyo vimepimwa vinauzwa kwa bei kubwa kuanzia shilingi milioni nne hadi milioni 14 bei ambayo vijana na wananchi wanashindwa kumudu gharama zake.
Diwani wa kata ya Njombe Mjini Agrey Mtambo amesema sababu inayofanya vijana na wananchi wengine kushindwa kununua viwanja hivyo ni gharama kuwa kubwa na kuiomba halmashauri ijaribu kupunguza bei ya Viwanja ili Vijana na wananchi wengine wenye uwezo wa chini wanufaike navyo.
Akijibu maswali ya vijana hao kuhusiana na Viwanja hivyo afisa ardhi wa halmashauri ya mji wa Njombe Thadei Kabonge amesema viwanja hivyo havikugawiwa kwa upendeleo wowote bali viliuzwa kwa kila mmoja mwenye uwezo wa kuvinunua Huku mkurugenzi akisema mwaka 2012 viwanja vilipimwa ambapo bado hadi sasa vingine havijapata watumiaji .
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Luth Msafiri ameagiza halmashauri hiyo kutoa viwanja vyote kwa wananchi na kuwatangazia wananchi kwamba viwanja vimekwisha na vimeuzwa kwa utaratibu wa serikali ambapo ameshindwa kuridhika na majibu ya Afisa ardhi wa Mji kwamba tangu wapime mwaka 2012 ikiwa ongezeko la watu lipo kila mwaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment