KATIBU MKUU CHADEMA TAIFA VINCENT MASHINJI AKISALIMIANA NA BIBI MAGDALENA WA RAMADHANI NJOMBE ALIPOTEMBELEA KUKAGUA MIRADI YA VYOO NA VIBANDA VYA BIASHARA VINAVYOJENGWA KWENYE MTAA HUO VIKIWA CHINI YA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA BATHROMEO KYANDO ALIYECHAGULIWA KUPITIA TIKETI YA CHADEMA.
HAPA KATIBU MKUU AKIZUNGUMZA NA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE {CHADEMA} LUCIA MLOWE WAKIWA KWENYE MRADI WA VIBANDA VYA BIASHARA UNAOTEKELEZWA MTAA WA RAMADHANI.
HIVI NI VYOO AMBAVYO VIMEJENGWA CHINI YA USIMAMIZI WA MWENYEKITI HUYO ALIYETEMBELEWA NA VIONGOZI CHADEMA TAIFA.
HIVI VYOO NDIVYO VILIVYOKUWA VIKITUMIKA KABLA YA VIPYA KUKAMILIKA
MBUNGE WA IRINGA MJINI CHUNGAJI PETER MSIGWA AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA RAMADHANI NJOMBE MJINI
VIBANDA HIVYO VYA SERIKALI YA MTAA WA RAMADHANI AMBAVYO NI MRADI WA SERIKALI NA KATIKATI NI JENGO LA OFISI YA MTAA NALO LINANDELEA KUJENGWA LAKINI LIMEPAULIWA.
SHANGWE NA NDEREMO ZA AKINAMAMA WAKISHANGILIA KWA FRAHA BAADA YA KUTEMBELEWA NA VIONGOZI CHADEMA TAIFA.
HAPA NI ENEO LA KIWANJA CHA OFISI YA CHADEMA MKOA INAPOTARAJIA KUJENGWA
KATIBU CHADEMA MKOA WA NJOMBE ALATANGA NYAGAWA AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA KATIBU MKUU CHADEMA TAIFA.
MBUNGE VITI MAARUMU MKOA WA NJOMBE LUCIA MLOWE AKIMSIKILIZA KATIBU KWA UMAKINI.
KULIA NI DIWANI WA KATA YA RAMADHANI NA KUSHOTO NI MBUNGE VITI MAALUMU MKOA LUCIA MLOWE WALIWA ENEO LA KIWANJA CHA OFISI YA CHADEMA MKOA WA NJOMBE LUNYANYWI.
MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE TAIFA HASHIMU JUMA ISSA AKIZUNGUMZA NA WANANJOMBE.
AKINA MAMA WA NJOMBE WAKIWA NA FRAHA KUBWA
HILI NI ENEO LA UKUMBI WA MLIMANI MOTEL
MADIWANI WAKISIKILIZA KWA UMAKINI AKIWEMO DIWANI WA KATA YA RAMADHANI GEOGE MENSON SANGA KULIA
KATIBU MKUU CHADEMA TAIFA VINCENT MASHINJI AKIZUNGUMZA NA WANA NJOMBE KATIKA UKUMBI WA MLIMANI MOTEL
MWANASHERIA WA KUJITEGEMEA ENOS SWALE AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA WANA LUPEMBE
NJOMBE
Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Taifa Dr. Vincent Mashinji ametembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya vyoo na vibanda vya biashara vilivyopo Mtama wa Ramadhani Mjini Njombe.
Dr. Mashinji amepongeza Serikali ya mtaa wa Ramadhani akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtama huo Bathromeo Kyando na Diwani wake George menson Sanga waliochaguliwa kupitia CHADEMA kwa kutekeleza miradi Mkubwa ukiwemo wa vyoo ulioghalimu zaidi ya shilingi milioni 30 na vibanda vya Serikali ya Mtama ambavyo vinaendelea kujengwa.
Mradi huo unaosimamiwa na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa iliyopo chini ya CHADEMA umefiki hatua za nzuri na utakamilika muda wowote kuanzia sasa.
Dkt Mashinji amewataka viongozi wengine kuiga mfano wa Serikali ya Mtama wa Ramadhani kutekeleza miradi hiyo ili mwaka 2020 waweze kuwa na nafasi ya kupata ushindi kuanzia kwenye ngazi za mitaa hadi taifa.
Aidha Dr. Mashinji amemtaka Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Njombe Lucia Mlowe wa CHADEMA kushikamana na viongozi wa kata na vijiji ili kuboresha miundombinu iliyopo huku na kumpongeza kwa jitihada alizozianza za kununua kiwanja eneo la Hagafiro na kuanza ujenzi wake.
Kuhusu Wazee Dr. Mashinji amesema Serikali inatakiwa kuwaboreshea huduma za matibabu bure na kuongeza madawa kwenye mahospitali ili watu wote wapate huduma za matibabu kwa uhakika huku swala la elimu bure lililotangazwa na Serikali likibaki kuwa tatizo kwa kushindwa kutekeleka kama Ahadi iliyotolewa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Hashimu Juma Issa amesema CHADEMA Mkoa wa Njombe ni mfano wa kuigwa kwa kuwa na muamko wa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutoka CHADEMA Njombe zijenge ofisi zao na kuondokana ofisi za kupanga kwa kujenga za kwao kama ilivyoanza kujenga ofisi ya chadema mkoa.
Nae Katibu CHADEMA Mkoa wa Njombe Alatanga Nyagawa akiwa na Mwenyekiti wake Fakii Lulandala wamesema Mkoa wa Njombe umejipatia ushindi kwa kata za Mjini zote ambazo zimeonekana kufanya vizuri kuliko waliokuwepo madiwani waliopita wa CCM ambapo wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanashinda kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 kwa kushinda majimbo na mitaa na kata za Njombe na Wilaya zake.
No comments:
Post a Comment