MILANGO YA VYOO VYENYE MATUNDU 8 KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA ANNE MAKINDA ILIYOPO KATA YA IHANGA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIONJA CHAKULA CHA WANAFUNZI WA ANNE MAKINDA ALIPOTEMBELEA
KULIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI KATIKATI NI MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA ANNE MAKINDA VERONICA MLOZI NA WA KUSHOTI NI AFISA ELIMU SHULE ZA MSINGI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE ZEGELI SHENGERO
HUYU NI MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI MUUNGANO ILIYOPO KIFANYA MWALIMU BABTIST SARUFU AKIZUNGUMZA NA MKUU WA WILAYA AKIWA OFISINI KWAKE
HII NI NYUMBA YA MWALIMU NA HAWA NI WANAFUNZI WANAJIUNZA KILIMO SHULENI
NYUMBA MPYA YA MWALIMU IMEGHALIMU MILIONI TATU NA NGUVU ZA WANANCHI WA KIFANYA
HII NI ZAHANATI YA KIFANYA AMBAYO MKURUGENZI AMESEMA KWA KUWA VITANDA HAVITUMIKI ATAKWENDA KUHAMISHA NA KUPELEKA SEHEMU ZENYE UHITAJI WA VITANDA
PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA WILAYA MKURUGENZI,MAAFISA ELIMU HASSAN IGWE,ZEGELI SHENGERO NA KATIBU TAWALA NA ASKALI WA POLISI
NJOMBE
Halmashauri ya Mji wa Njombe imetakiwa kusimamia vizuri pesa zinazopelekwa kwaajili ya elimu bure kwa kukarabati madarasa yaliochimbika sakafu ili yawe na viwango vinavyokubalika pamoja na nyumba za walimu zinazoendelea kujengwa .
Bi.Msafiri ametoa agizo la kukarabati vyumba chakavu vya madarasa kupitia pesa za elimu bure zinazotolewa na serikali na kuwahamishia chumba chenye hewa ya kutosha wanafunzi wa darasa la awali peluhanda ambapo akiwa shule ya msingi Muungano ya Kifanya ameagiza kuondolewa milango iliyopo chini ya kiwango kwaajili ya nyumba ya mwalimu.
Akiwa katika shule ya sekondari ya wasichana ya Anne Makinda Bi.Msafiri amekagua miradi ya nyumba za walimu na choo chenye matundu 8 kilichogharimu shilingi milioni 16 huku nyumba ya walimu ikitarajia kughalimu shilingi milioni 150 hadi kukamilika kwake na kufanya jumla ya shilingi milioni 166.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Bi.Iluminata Mwenda amesema darasa la awali lipo kujengwa ambapo ameomba wananchi kuanza kusogeza tofari elfu hamsini ili Halmashauri iwaunge mkono kwa kupeleka milioni 22 Kwaajili ya darasa hilo ambapo akiwa zahanati ya kifanya ameahidi kuondoa vitanda visivyotumika na kupeleka kungine.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Luth Msafiri ametembelea shule ya msingi Mpeto iliyopo kata ya Ramadhani,Shule ya msingi peluhanda iliyopo kata ya Mjimwema,Kituo cha kukusanyia matunda kilichopo Nundu kata ya Yakobi,Shule ya wasichana ya Anne Makinda iliyopo kata ya Ihanga na Zahanati ya Kifanya na shule ya msingi Muungano ya Kifanya.
No comments:
Post a Comment