AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA HAVANGA LIVIN JOHN AKISOMA TAARIFA FUPI MBELE YA MBUNGE HUYO
MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM WILAYA YA NJOMBE BI.VELONICA AKIZUNGUMZA NA KUWASHUKURU WANANCHI KWA KUKICHAGUA CHAMA HICHO KUANZIA NGAZI YA WENYEVITI WA VIJIJI HADI RAIS KWENYE JIMBO HILO
MBUNGE AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA HAVANGA
MBUNGE AMESHIKA MPIRA WA KUWAPATIA VIJANA WAENDELEZE MICHEZO
VIFAA VYA MICHEZO MBUNGE HONGORI AKIKABIDHI KWA VIJANA WA KIUME NA WA KIKE
KIONGOZI WA TIMU YA MPIRA WA MIKONO KUTOKA KIJIJI CHA HAVANGA AKITOKA BAADA YA KUPOKEA MPIRA NA MBUNGE IULI WANAWAKE NAO WASHIRIKI MICHEZO
WANANCHI WALIOFIKA KWENYE MKUTANO HUO WAKISIKILIZA KWA UMAKINI
MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA HAVANGA BWANA PHILIMON DAUD MUMUSI AKIFUNGUA MKUTANO
MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMBE JORAM HONGORI AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA HAVANGA KUHIMIZA WAJIUNGE NA MFUKO WA CHF
NJOMBE
Wananchi Wilayani Njombe wametakiwa kujiunga
na mfuko wa taifa wa afya CHF Kwaajili
ya kupata huduma za matibabu kwa
kuchangia shilingi elfu kumi kwa mwaka ili kunufaika na matibabu bure kupitia mfuko huo.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Lupembe
Joram Hongori wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea vijiji na kata za jimbo
hilo kukagua miradi na kushukuru wananchi kwa kumchagua na kusema kuna umihimu
mkubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa kuchangia shilingi elfu kumi kwa
mwaka.
Mwalimu Hongori amesema viongozi wa serikai za
vijiji wanatakiwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo huku akisema swala
la kukosekana kwa dawa kwenye vituo vya afya,zahanati na hospitali serikali ina
mpango wa kuanzisha maduka maalumu karibu na hospitali ili kuhakikisha kila
mwananchi ananunu dawa kwa bei ya ruzuku pindi dawa zinapokuwa zimekosekana
hospitralini.
Awali akisoma
taarifa fupi mbele ya Mbunge huyo afisa mtendaji wa kijiji cha Havanga kata ya
kidegembye Livin John amesema wananchi wa kijiji hicho wanakabiliwa na
changamoto ya ujenzi wa zahanati ambayo walikwisha kuanza ujenzi wake.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Havanga
wamelalamikia kuvunjwa kwa jengo la zahanati walilokwisha kamilisha ujenzi wake
kutokana na uzembe wa mhandisi wa Wilaya hiyo kushindwa kwenda kukagua
maendeleo yake na kusababisha kujengwa tofauti na viwango vya halmashauri ikiwa
ramani alipeleka mwenyewe.
Katika kuunga mkono
jitihada za wananchi wa kijiji cha havanga za kujenga zahanati hiyo mbunge wa
jimbo la lupembe ameahidi kuchangia shilingi laki tatu kwaajili ya kusombea
mawe ya kujengea msingi ili kusukuma maendeleo ya kijiji na kuboresha huduma za
afya.
No comments:
Post a Comment