CHUMBA CHA WODI LA DARAJA LA KWANZA LA HOSPITALI YA KIBENA NAMNA KILIVYOCHAKAA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA WADAU BAADA YA KUZINDUA UKARABATI WA JENGO LA WODI GRAD 1
ELLY NGOLE BAADA YA KUMSOMEA TAARIFA FUPI MKUU WA WILAYA SASA WANAENDELEA NA MAZUNGUMZA KUHUSIANA NA UKARABATI HUO
HAPA MKUU WA WILAYA ANAKABIDHIWA VIFAA VYA UJENZI AMBAVYO NI RANGI
MWENYEKITI WA KAMATI YA AFYA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE FILOTEUS MLIGO MWENYE KOTI LA SUTI NA WA KATIKATI NI ELLY NGOLE MDAU WA AFYA NA ALIYEFUNGA KILEMBA NI MKUU WA WILAYA AKIPOKEA KOPO LA RANGI AKIWA NJE YA WODI HILO LA HOSPITALI YA KIBENA.
RAYMOND MBOGAILONGWE AKIPEANA MKONO NA MKUU WA WILAYA LUTH MSAFIRI BAADA YA KUKABIDHI VIFAA HIVYO
HUU NI UCHAKAVU WA CHUMBA CHA WAGONJWA KIBENA HOSPITALI
VYOO NAVYO HAVIKO SALAAMA VIMEHARIBIKA VIBAYA KAMA UNAVYOSHUHUDIA HAPO
PICHA YA PAMOJA NA WADAU WANAOSHIRIKI KUKARABATI WODI HILO LA DARAJA LA KWANZA BAADA YA NDUGU YAO SE SWALE KUPEWA HUDUMA ZA MATIBABU VIZURI NA HATIMAYE KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MHIMBILI ANAKO ENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
HILI NDILO WODI LA DARAJA LA KWANZA LA KIBENA AMBALO LINAANZA KUFANYIWA UKARABATI NA BAADHI YA WADAU WA AFYANJOMBE MJINI.
NJOMBE
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Luth Msafiri jana amezindua zoezi la ukarabati
wa wodi la daraja la kwanza katika
hospitali ya Kibena lenye vyumba 8 ambao unatarajia kuanza juma tatu
Octoba 3 mwaka huu.
Akizungumza na wadau wa afya mjini Njombe ambao wamejitoa
kukarabati Wodi hilo Bi. Msafiri
amewapongeza kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za
afya .
Bi.Msafiri ametumia fursa hiyo kumuagiza mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Njombe kuhakikisha Mhandisi wa ujenzi anashilikiana na
wadau hao na kupeleka tathmini ya ukarabati huo ofisini kwake jumatatu asubuhi.
Akisoma taarifa fupi kwa niaba ya wadau wengine wa
afya Elly Ngolly amesema wazo la kukarabati wodi hilo lilitoka kwa Raymond
Mboga Ilongwe na baadaye Stivin Njowoka baada ya ndugu yao mama Se swale kupata
huduma nzuri za matibabu na kupelekwa Muhimbili.
Afisa utumishi akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa
halmashauri ya mji wa Njombe Gualbat
Mbujilo ameshukuru wadau kwa kusaidia ukarabati huo na kwamba
halmashauri inaendelea na ukarabati wa maabara huku mwenyekiti wa kamati ya
huduma za afya Filoteus Mligo akiomba wadau wengine kuendelea kujitokeza
kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili hospitali ya kibena.
No comments:
Post a Comment