Mgeni
rasmi kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Otilia Gowelle akizindua Mkutano Mkuu wa kwanza wa wataalamu
wa tiba ya dharura Tanzania ambao unafanyika leo katika ukumbi wa LAPF
jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umelenga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa
washiriki mbalimbali kutoka katika sekta ya afya nchini. Kutoka kushoto
ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga, Mkurugenzi
wa ABBOT Fund nchini, Natalia Lobue, Rais wa Chama cha Madaktari na
Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT), Dk Hendry Sawe, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa
Lawrence Museru, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi na Mkuu wa Kitivo cha Tiba,
MUHAS, Profesa Sylvia Kaaya.
Baadhi
ya washiriki wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi leo katika mkutano
unaoendelea katika ukumbi wa LAPF jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwasilisha mada leo kwenye mkutano huo leo.
Washiriki wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Lawrence Museru wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano huo leo.
Rais
wa Chama cha Madaktari na Wataalamu wa Tiba ya Dharura Tanzania (EMAT),
Dk Hendry Sawe akiwasilisha mada kwenye mkutano huo leo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mkutano huo Leo. |
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mkutano huo Leo.
Katibu
wa Chama Cha Madaktari Walio Katika Mafunzo ya Ubingwa wa Dharura
Afrika, Dk Peter Mabula akitoa mafunzo ya kuokoa maisha ya watu kwa
washiriki mbalimbali. Mafunzo hayo yalianza juzi katika Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi-Muhimbili (MUHAS).
Washiriki
wakimsikiliza Dk Mabula wakati akiwasilisha mada juu ya kuokoa maisha
ya watu wanaopata magonjwa ya dharura na ajali juzi.
Washiriki
wakijifunza kwa vitendo jinsi ya kuokoa maisha ya watu wanaopata
magonjwa ya dharura na ajali. Mafunzo hayo yalifanyika juzi katika
ukumbi wa MUHAS.
No comments:
Post a Comment