Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, August 12, 2016

USAFIRI WA BAJAJI WAREJEA BARABARANI


Usafiri wa bajaji Umerejea Barabarani Baada Ya Kugoma Kuchukua Abiria Kwa Siku Tatu  Kutokana Na Kuzuiliwa Wasitumiye  Barabara Kuu Ya Njombe Songea Badala Yake Watumiye Za Mitaani.

Hatua Hiyo Ya Kugomea Kwa Muda Huo Imekuja Ikiwa Ni Siku Tatu Zimepita Tangu Kikao Kifanyike  Na Maafisa Usalama Wa Barabarani Kutoa Maelekezo Njia Zilizoanishwa Kisheri Kutumia  Bajaji Na Hice.

Madereva Bajaji Wamewatuhumu Madereva Wa Hice Kwamba Wanawaondoa Barabarani Ili Biashara Ifanywe Na Wao Ikiwa Wote Wanatafuta Riziki Alisema Mwenyekiti Bajaji Wilaya Ya Njombe Bwana Phedrick Kabelege  Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari.

Nao Madereva Wa Gari Aina Ya Hice Walipohojiwa Na Waandishi Wa Habari Wakatupia Lawama Bajaji Kwamba Haziko Kisheria Na Hivyo Hastahili Kuwepo Barabarani Kwani Mwenye Haki Na Hice Ambapo Mvutano Huo Unaendelea Hadi Sasa Licha Ya Vyombo Vyote Kuendelea Kufanya Kazi.

No comments:

Post a Comment