Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, August 11, 2016

RC NJOMBE AZINDUA MTANDAO WA WAKULIMA WA PARACHICHI LEO



 MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIKAGUA PARACHICHI ZILIZOPANDWA NA BAADHI YA WAKULIMA WA KATA YA RAMADHANI


 MKUU WA MKOA NJOMBE AKISALIMIANA NA  MAKAMU MWENYEKITI WA CCM  AKIWA NI MIONGONI MWA WAKULIMA  WA KUTOKEA KIJIJI CHA IMALINYI





 HAPA MKUU WA MKOA AKIWA MGENI RASMI AKIWA NA TIMU NZIMA YA VIONGOZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA WAKIKAGUA SHAMBA HILO




 MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA PHILIP MANGULA AKISALIMIA WAKULIMA WENZAKE
 JOHANNES  KAMONGA AKITOA NASAHA ZAKE KWA WAKULIMA
 ERASTO NGORE MKULIMA  NA NI MRATIBU WA MTANDAO WA WAKULIMA WA PARACHICHI MKOA WA  NJOMBE AKIZUNGUMZIA CHANGAMOTO INAYOWAKABILI WAKULIMA WA ZAO HILO






 HAYA NDIYO MAPARACHICHI  YA ITULIKE



MKUU WA MKOA WA KATIKATI DKT REHEMA NCHIMBI,kUSHOTO nI mKUU wA WILAYA YA NJOMBE RUTH MSAFIRI NA WA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA MAKETE VERONICA KESSY.

Mkuu Wa Mkoa  Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Leo Amezindua Mtandao Wa  Wakulima  Wa Parachichi Mkoa  Ambapo  Amerudia Kauli Yake Kwa Wakurugenzi Na Watendaji  Kuongeza Kasi Ya Upandaji Wa Miti Ya Matunda  Ya Parachichi.

Akizungumza Na  Mtandao Wa Wakulima Wa Matunda Aina Ya  Parachichi Mkoa Wa Njombe Dkt Nchimbi  Amewaagiza Wakuu Wa Wilaya Za Mkoa Huo Kuhakikisha Wanakwenda Kusimamia   Utengaji Wa Maeneo  Kwaajili Ya Vijana  Watakaojiajiri Kwenye Kilimo Cha  Parachichi  Kwaajili Ya Kuinua Uchumi Wao.

Dkt Nchimbi Amesema  Kuzinduliwa Kwa Mtandao Wa Wakulima Wa Parachichi Mkoa Wa Njombe Ni Sawa Na Kuzindua Ajira Kwa Vijana  Na  Kuongeza Ufanisi, Kuinua Uchumi Na Maendeleo Kutokana Na  Wakulima Wa Parachichi  Kwa Manufaa Yao Na Taifa Zima.

Amesema Anategemea Kila Mkulima Wa Parachichi Atanufaika Na Kilimo Hicho Kwa Kujiunga Kwenye Mfuko Wa Bima Ya Afya CHF
  Baada Ya Miaka Miwili Ambapo  Kuzinduliwa Kwa Mtandao Huo Kunatoa Nafasi Kwa Wakuu Wa Wilaya Kukagua Kila Halmashauri Kama Imetekeleza Agizo Lake La Kulima Ekari  Kumi  Na Ekali Moja Kwa Kila Shule.

Akisoma Taarifa Fupi Mbele Ya Mgeni Rasmi Kwa Niaba Ya Mtandao Wa Wakulima  Wa Parachichi  Weisy Wikedzi  Amesema Mtandao Huo Ulianza Mwaka 2012 Ukiwa Na Vikundi Vitano  Vyenye Wanachama Mia 916 Ambavyo Vina  Hekta  Mia 341.236 Zenye Miti  Zaidi Ya Elfu 85  Ya Parachichi.

Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Baadhi Ya Wakulima Kutoka Halmashauri Sita Za Mkoa Wa Njombe  Wa Makete,Ludewa,Wanging'ombe Na Njombe  Wamepongeza Kwa Hatua Ambayo Imefikia Ya Mtandao Wa Wakulima Wa Parachichi  Ambapo Wamesema Kwa Sasa Soko Linapatikana Kwa Uhakika  Huku Wakiomba Serikali Kusaidia Kuzuia Baadhi Ya Madalali Na Wafanyabiashara Wanaonunua Kwa Rumbasa.



No comments:

Post a Comment