Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) akiwa pamoja na wadau
wengine wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuangalia Maandalizi ya
Jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
lililopo kwenye Shule ya Sheria Sinza leo jijini Dar es salaam. Baadhi
ya Wadau wa Mahakama waliotembelea Mahakama hiyo ni Wizara ya Katiba na
Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mawasiliano, Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu
Wakuu na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau
wa Mahakama ya Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya
Jengo litakalotumika kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi leo Sinza jijini Dar es salaam. Anayetazamana na Kattanga ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na
anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi Bibi Maimuna Tarishi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga (kulia)
wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo
litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi
leo jijini Dar esa salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba
na Sheria Prof. Sifuni Mchome (Kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi wakizungumza
jambo walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya uanzishwaji wa
Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es
salaam
No comments:
Post a Comment