WA KWANZA KUTOKA KUSHOTO NI DIWANI WA KATA YA KICHIWA PETER NYAHUYA WA KATIKATI NI MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMBE JORAMU HONGORI NA WA TATU KUTOKA KUSHOTI NI KATIBU WA CCM VIJANA WILAYA YA NJOMBE
WANANCHI WA IKANDO WAKIMSIKILIZA MBUNGE WAO
MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA IKANDO BWANA MWINAMI AKIFUNGUA MKUTANO MARA BAADA YA MBUNGE KUWASILI
MBUNGE WA LUPEMBE JORAMU HONGORI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA IKANDO
Serikali Imetenga Jumla Ya Shilingi Tririon 29.5 Kwaajili Ya Kuanzisha Miradi Mbalimbali Itakayo wasaidia Wananchi Kufikia Uchumi Wa Kati Huku Asilimia 40 Zikienda Kwenye Mipango Ya Miradi Ya Maendeleo Ya Afya,Umeme, Elimu Miundombinu.
Mbunge Wa Jimbo La Lupembe Joramu Hongori Akizungumza Na Wananchi Wa Vijiji Vya Kata Ya Kichiwa Ikando,Ibumila Na Kichiwa Amesema Pia Serikali Imetenga Kiasi Hicho Cha Tririon 29.5 Kwaajili Ya Uwekezaji Wa Viwanda ,Kuongeza Uzarishaji Kwenye Kilimo Katika Kipindi Cha Miaka Mitano.
Hongori Amesema Mpango Wa Serikali Katika Kilimo Ni Kushusha Bei Ya Pembejeo Za Kilimo Ikiwemo Mbolea Za Kwenye Maduka Ya Watu Binafsi Na Zile Za Ruzuku Ili Kila Mkulima Awe Na Uwezo Wa Kununua Pembejeo Hizo Kwa Wakati Wake.
Amesema Serikali Haitaweza Kuagiza Mbolea Kutoka Nje Ya Nchi Badala Yake Itachukuliwa Kwenye Viwanda Vya Ndani Ya Nchi Huku Wizara Ya Kilimo Kwa Kushirikiana Watafiti Wa Udongo Wakiwa Na Jitihada Za Kutafiti Udongo Unaotakiwa Kwa Kilimo Na Kwamba Tayari Wamebaini Asilimia Kubwa Ya Udongo Unakosa Madini Ya Chokaa.
Awali Akimkaribisha Mbunge Huyo Diwani Wa Kata Ya Kichiwa Peter Nyahuya Amewambia Wananchi Kusitisha Zoezi La Kuchimba Na Kumwaga Kifusi Kwenye Barabara Iliyopo Kijijini Hapo Kutokana Na Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Kukubali Kwenda Kuwalimia Kwa Mitambo Licha Ya Kuwa Haitamwagiwa Maji Na Kushindiliwa.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Kijiji Cha Ikando Isack Mwinami Amesema Pamoja Na Kijiji Hicho Kukabiliwa Na Uharibifu Wa Miundombinu Ya Barabara Lakini Pia Kuna Tatizo La Kukosekana Kwa Huduma Za Maji ,Uharifu Kuongezeka Hususani Wizi Wa Mali Mbalimbali Na Kwamba Wanatarajia Kuanzisha Ulinzi Shilikishi Wakati Wowote Kuanzia Sasa.
No comments:
Post a Comment