Wednesday, July 6, 2016
WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WA NJOMBE LEO WAMEUNGANA NA WAISLAMU WENGINE DUNIANI KOTE KUSHEREHEKEA SKUKUU YA EID ELFITR
Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Mkoani Njombe Leo Wameungana Na Waumini Wengine Wa Dini Hiyo Duniani Kote Baada Ya Kutimiza Siku 29 Za Mfungo Katika Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Ambapo Wametakiwa Kuendelea Kumucha Mungu Na Kutekeleza Masharti Ya Nguzo Kuu Tano Za Uislamu.
Rai Hiyo Imetolewa Na Imamu Wa Msikiti Mkuu Wa Njombe Mjini Rajab Msigwa Wakati Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Mara Baada Ya Waumini Kumaliza Zoezi La Kuswali Na Kusema Kuwa Siku Ya Idd Ni Ya Kusherehekea Na Siyo Siku Ya Kumuasi Mwenyezi Mungu Wa Sulahana Watala Na Kwamba Wanasherehekea Uislamu Kwa Kuwakalibisha Wengine Kujiunga Na Dini Hiyo.
Imamu Msigwa Amesema Hategemei Muislamu Aliyefunga Kwa Siku 29 Akagundulika Akimkufuru Mungu Kwa Kutenda Maovu Nakwamba Waumini Hao Wanapaswa Kumucha Mungu Na Kuonesha Utii Pamoja Na Kuwa Na Moyo Wa Kujitolea Na Kusaidia Wasiyo Jiweza Kwa Kutoa Sadaka Ili Kukuza Imani Ya Uislamu Huku Wakitakiwa Kukemea Tabia Za Uharifu Wakati Wa Kusherehekea Skukuu Hiyo.
Amesema Nguzo Tano Zinatakiwa Kutekelezwa Wakati Wa Mfungo Wa Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Ikiwemo Kutoa Zaka,Kusimamisha Swala , Kuhiji Kwa Yule Mwenye Uwezo Wa Kwenda Kuhiji Na Kwamba Kufunga Katika Kipindi Cha Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani Ni Maandalizi Ya Kwenda Kuhiji Ambapo Kumaliza Sherehe Hizo Wengine Wanapaswa Kuendeleza Siku Sita Za Kumalizia Mwezi Mtukufu Ramadhani.
Kwa Upande Wao Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Akiwemo Aman Mohamed Gadau Wametaka Jamii Kushirikiana Na Waumini Hao Kusherekea Skukuu Ya Eid Elfitr Na Kuomba Ulinzi Na Usalaama Kuimalishwa Kila Mahali Huku Waumini Wakitakiwa Kuwalinda Watoto Wao Kwaajili Ya Kujihadhari Na Matukio Ya Ajali Na Uharifu Majumbani Mwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment