HILI NI GARI AMBALO LIMEKODIWA NA MDAU MMOJA WA KIJIJI CHA ISINDAGOSI JAMES MLIGO AMBAYE AMECHANGIA MILIONI TANO KWAAJILI YA KUJAZA KIFUSI KWENYE MADARAJA HAYO MAWILI KUWAUNGA MKONO WANANCHI HAO.
HILI NI DARAJA LA MTO MTITAFU AMBALO LINAUNGANISHA KATA YA ITULAHUMBA NA MDANDU LINALOSAIDIA KUVUKA KWENDA SHULE YA SEKONDARI WANIKE.
WANANCHI HAO WAKICHIMBA KIFUSI KWAAJILI YA DARAJA LA MTO MTITAFU BAADA YA KUKAMILISHA KUJAZA KIFUSI MTO WA KWANZA WA IDEGE ULIOPO KIJIJI CHA ITULAHUMBA KITONGOJI CHA WANIKE INAYOUNGANISHA KATA YA ITULAHUMBA NA MDANDU
HILI NI DARAJA LA MTO IDEGE AMBALO TAYARI LIMEKAMILIKA KUFUKIWA NA HAPA WANANCHI WANARUDI ZAO NYUMBANI KWAO
HUYU NI MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE ANTONY MAHWATA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA MADARAJA YANAYOLALAMIKIWA NA WANANCHI WA ITULAHUMBA NA KUSEMA KUWA MKANDARASI ALIYEKUWA AKITENGENEZA MADARAJA HAYO HAKUWA NA SIFA ZA KUTENGENEZA NA HIVYO HALMASHAURI IKALAZIMIKA KUMSIMAMISHA NA KUMUWEKA MWINGINE WA KUKAMILISHA.
MWENYE SUTI NYEUSI NI KAIMU MHANDIS WA UJENZI WILAYA YA WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE.
HILI NI JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE NDIPO MAZUNGUMZO BAINA YA VIONGOZI HAO NA WAANDISHI WA HABARI YALIFANYIKIA.
Na Michael Ngilangwa -Njombe
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Wameitaka Halmashauri ya Wilaya Hiyo Kumchukulia Hatua za Kisheria Mkandarasi Aliyetelekeza Mradi wa Ujenzi wa Madaraja Katika Mito ya Mtitafu na Dege Yanayounganisha Vijiji Vya Kata Itulahumba na Mdandu.
Wakizungumza na Waandishi wa habari Wananchi wa kijiji hicho Wamesema Ujenzi wa Madaraja Hayo Umetelekezwa Kwa Takribani Miaka Minne na Kusababisha Adha Kwa Wanafunzi na Wananchi Wanaotumia Barabara Hiyo Hasa Kipindi cha Masika Kutokana na Mito Hiyo Kujaa Maja na Kuharatisha Maisha Yao.
Kufuatia Adha Hiyo Wananchi Hao Wamamua Kuanza Ukarabati Katika Maeneo ya Madaraja Hayo Kwa Kumwaga Vifusi Kwa Nguvu Zao na Wadau wa Maendeleo wa Kata Hizo, Huku Wakiulalamikia Uongozi wa Halmashauri Hiyo Kwa Kushindwa Kukamilisha Ujenzi Huo.
Akitolea Ufafanuzi Kuhusu Ujenzi wa Madaraja Hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Antony Mahwata Amesema Ujenzi Utakamilika Ndani ya Wiki Mbili, Huku Kaimu Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri Hiyo Akielezea Hatua Walizochukua Baada ya Mkandarasi Kutelekeza Mradi Huo.
Aidha Bwana Mahwata Amesema Halmashauri Hiyo Inatarajia Kukamilisha Ujenzi Wa Madaraja Hayo Ndani Ya Wiki Mbili Kama Alivyomuahidi Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Na Kusema Wananchi Wa Itulahumba Wanatakiwa Kuwa Wavumilivu Wakati Matengenezo Yakifanyika Haraka Kwani Tayari Mkandarasi Amekwisha Kupatikana Wa Kukamilisha Madaraja Hayo Huku Akipongeza Wananchi Kwa Kazi Waliyoifanya Ya Kujaza Udongo Kwenye Eneo Hilo.
Kaimu Muhandis Wa Ujenzi Wilayani Wanging'ombe Boniface Kasambo Licha Ya Kutotoa Thamani Ya Madaraja Hayo Lakini Amesema Halmashauri Imelazimika Kumusimamisha Mkandarasi Wa Awali Baada Yakuwa Hanauwezo Wa Kukamilisha Miradi Hiyo Ambapo Sasa Wamempatia Mwingine Wa Kutekeleza Miradi Hiyo Aliyodai Imedumu Kwa Miezi Sita Na Siyo Miaka Miwili Iliyotwajwa Na Mwenyekiti Wa Halmashauri Huku Wananchi Nao Wakisema Ni Miaka Minne Sasa.
Hivi Karibuni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi Aliuagiza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuhakikisha Wanakamilisha Ujenzi wa Madaraja Hayo Ili Kuwaondolea Adha ya Miundombinu ya Usafiri Wananchi wa Itulahumba na Mdandu.
No comments:
Post a Comment