Wajumbe
wa Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto , Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa n
Hesabu za Serikali ya India, Bw. Shashi Kant Sharma, Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza, Sir Amyas Morse, na
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania, Prof.
Mussa Juma Assad, wakitia saini zao katika ripoti 11 za ukaguzi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo
wakati wa mkutano wake wa sabini (70), uliofanyika siku ya jumanne
hapa Makao Makuu ya Umoja huo, New York, Marekani. Ripoti hizo ni
matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa na Wajumbe wa Bodi ya
Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza Sir Amyas Morse ambaye
amemaliza muda wake wa uhudumu wa miaka sita katika Bodi hiyo. Hafla
hiyo ilihusisha pia kukaribishwa kwa Bw. Kay Scheller Rais wa Ofisi
Kuu ya Ukaguzi ya Ujerumani anayechukua nafasi ya Uingereza.
Mabadilishano hayo yalikuwa ni sehemu ya Kikao cha 70 cha Bodi ya
Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa ambayo ipo chini ya Uenyekiti wa Prof
Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka
Tanzania. Kutoka kushoto ni: Bw. Kay Scheller ( Ujerumani), Sir Amyas
Morse ( Uingereza), Katibu Mkuu Ban Ki Moon ( UN), Prof Mussa J. Assad(
Tanzania) na Bw. Shashi Kant Sharma ( India).
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, Prof. Mussa Assad akizungumza
wakati wa hafla ya kuiaga Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali ya Uingereza ambaye amemaliza ujumbe wake wa miaka sita katika
Bodi. Mwenyekiti alitumia fursa hiyo kumshukuru Sir Amyas Morse kwa
ushirikiano na weledi mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi.
Ujumbe
wa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG)
muda mfupi kabla ya kuanza rasmi kwa kikao cha 70 cha Bodi ya Ukaguzi
ya Umoja wa Mataifa. Kutoka kushoto Bw. Isaya Jeremiah, Naibu Mkurugeni
Ukaguzi wa Nje, Bw. Jerome Francis, Naibu Mkurugenzi Ukaguzi wa Nje,
Bw. Salhina Mkumba, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Nje, na wa mwisho ni
Bw. Athuman S. Mbuttuka, Naibu Mkaguzi Mkuu anayesimamia ukaguzi wa
Hazina na Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum, New York.
Bodi
ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ambayo Mwenyekiti wake ni Mkaguzi
na Mdhibiti n Mkuu wa Hesabu za Serikali, ( CAG) Profesa Mussa J.
Assad jana ( Jumanne) imerejea na kuidhinisha ripoti kumi na moja
za Mashirika, Mifuko na shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Katika
kikao hicho cha 70 kilichofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, pamoja na kuidhinisha ripoti za Mashirika na Mifuko
iliyochini chini ya Umoja wa Mataifa, pia Bodi ilipokea taarifa
mbalimbali za kiutendaji zinazohusiana na majukumu ya Bodi hiyo.
Wajumbe
wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ni Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu wa Serikali ya India, Bw. Shashi Kant Sharma,
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Uingereza, Sir Amyas
Morse, na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Prof. Mussa J. Assad.
Pamoja
na kupitia na kuridhia ripoti hizo kumi na Moja, na kupokea taarifa
za kiutendaji, shughuli nyingine iliyofanywa na Bodi ya Ukaguzi
ilikuwa ni pamoja na kuiaga Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza baada ya
kumaliza kipindi chake cha miaka sita ya uhudumu katika Bodi hiyo.
Hafla
ya kuagwa kwa Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza ilihudhuriwa na Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki Moon pamoja na wadau mbalimbali
ambao ni wateja wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.
Nafasi
ya Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza imechukuliwa na Ofisi ya Ukaguzi ya
Ujerumani ambayo imekaribishwa rasmi kuwa mjumbe wa Bodi hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kuiaga ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza na
kuikaribisha Ofisi ya Ukaguzi ya Ujerumani, Mwenyekiti wa Bodi,
Prof. Mussa Assad amemshukuru Sir. Amyas Morse kwa mchango wake yeye
binafsi na Ofisi yake kwa uwajibikaji mkubwa na weledi wa hali ya juu
ambao umefanikisha utekelezaji wa mamlaka na majukumu ambayo Bodi hiyo
imekabidhiwa na Umoja wa Mataifa.
Akiikaribisha
Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Ujerumani, Prof. Assad
ameelezea matumaini yake ya kufanya kazi kwa karibu na ushirikiano wa
hali ya juu na mjumbe huyo ili kwa pamoja waweze kutekeleza majukumu
na mamlaka waliyokabidhiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Bodi
ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ilianzishwa mwaka 1946 na Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukagua hesabu za Mashirika, Mifuko
na Taasisi nyingine zilizo chini ya Umoja wa Mataifa, ili pamoja na
mambo mengine kuhakikisha kwamba Taasisi hizo zinatekeleza majukumu yake
kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja
na matumizi yenye tija na adilifu ya bajeti kulingana na mamlaka ya
Mashirika na Taasisi hizo.
Bodi
ya Ukaguzi inatekeleza majukumu yake kama chombo huru na taarifa zote
za ukaguzi huwasilishwa kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na
wateja ambao wanakaguliwa na Bodi hiyo.
No comments:
Post a Comment