Baadhi
ya wanafunzi tuliosoma Shule ya Sekondari Bwawani tukiwa katika picha
ya pamoja wakati wa kuelekea kuitembelea shule yetu hiyo..
Mwalimu
Leornad Chintowa akiwakaribisha baadhi ya wanafunzi waliopata kusoma
katika shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi la Magereza
nchini mara baada ya kuwasili kwa waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo
mapema leo.
Baadhi
ya waliokuwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bwawani iliyopo mkoa wa
Pwani wakipata maelekezo kutoka Kwa viongozi wa wanafunzi kuhusiana na
Maabara mpya iliyojengwa shule hapo kipindi ambacho waliokuwa wanafunzi
katika shule hiyo hawakuiacha.
Wanafunzi
wa shule ya sekondari ya Bwawani wakipiga picha na aliyewahi kuwa
mwanafunzi wa shule hiyo na kuhitimu mwaka 2004, Christopher Mwansasu
mara baada ya waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo kutembelea shule yao
kwaajili ya kuwatia moyo na amasa ya kusoma vijana wanaoendelea na
masomo shule hapo
Baadhi
ya wanafunzi waliowahi kusoma Shule ya Bwawani na kuishi katika Bweni
la Nguvu Kazi wakiwa mbele ya bweni walilowahi kuishi miaka hiyo wakiwa
shuleni hapo. Kutoka kulia ni Amosi Kilindo ambaye alihitimu kidato cha
nne shuleni hao mwaka 2004 na anayefuata ni Peter Mloka ambaye alihitimu
kidato cha Nne mwaka 2005.
Aliyewahi
kuwa mchezaji wa netball wa timu ya shule ya Bwawani kuanzia mwaka 2003
hadi mwaka 2006, Maria Plantana akimkabidhi mchazaji wa netball wa timu
ya shule ya bwawani Kwa sasa mpira wa Netball ikiwa kama zawadi ya
kuwatembelea wanafunzi hao shuleni hapo.
Maelekezo yakiendelea kwa waliokuwa wanafunzi wa shule ya Bwawani iliyopo Mkoa wa Pwani.
Aliyekuwa
Mwanafunzi wa Shule ya Bwawani, Salome Mathew akipanda Mti kama ishara
ya kumbukumbu shule hapo mara baada ya kuwasili shuleni hapo kwaajili ya
kuwatia moyo wanafunzi wanaoendelea na masomo
Kaka
Mkuu msaidizi (Mwenye sare) akibadilishana mawazo na waliokuwa
wanafunzi katika shule hiyo wakati walipotembelea shule hiyo kwaajili ya
kuwatia moyo na amasa wanafunzi wanaoendelea na Masomo katika shule
hiyo ya Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini Tanzania
wanaoshuhudia Pembeni ni walimu wa shule hiyo
Baadhi
ya wanafunzi wanaoendelea na masomo shule hapo wakiwa katika Picha ya
Pamoja na walimu na baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika Shule
hiyo ya Bwawani miaka kadhaa iliyopita.
Baadhi
ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita wakiwa katika bwalo la
shule kwaajili ya kuwasikiliza waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo miaka
kadhaa iliyopita ambao waliwatembelea na kuongea nao machache ikiwemo
kuwapa moyo na kuwafanya waone umuhimu wa shule pindi wanapokuwa
shuleni.
Baadhi
ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya Bwawani iliyopo Mkoa wa
Pwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea sehemu
mbalimbali za shule hiyo kujionea tofauti
Mmoja
wa wanafunzi aliyehitimu mwaka 2006, Frank Mushi akipanda Mti mara
baada ya kuwasilini shule hapo wakati wa ziara iliyofanya na wanafunzi
waliohitimu katika shule ya bwawani huku baadhi ya wanafunzi hao
waliowahi kusoma hapo wakitoa zawadi ya mipira kama vile mpira wa miguu,
wavu na mpira wa pete, huku wakitoa Miche 30 ya miti ambayo imepandwa
shule hapo kama ishara ya kumbukumbu kwa wanafunzi hao
Baadhi
ya wanafunzi waliosoma na kuhitimu katika shule ya Sekondari Bwawani
iliyopo Mkoani Wa Pwani wakiepelekwa kujionea ujenzi wa majengo
mbalimbali yanayoendelea kujengwa shule hapo yakiwemo mabweni ya
wanafunzi.Picha zote na Josephat Lukaza – Lukaza Blog
Hatimaye
waliowahi kusoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari ya Bwawani
iliyopo Mkoa wa Pwani wamefanikisha adhma yao ya kuitembelea iliyokuwa
shule yao kwaajili ya Kuwatia moyo na amasa vijana wanaoendelea na
masomo katika shule hiyo huku wengi wao wakiwa ni vijana wa kidato cha
Kwanza hadi cha Nne.
Waliowahi
kuwa wanafunzi hao waliwasili majira ya saa sita mchana na kupokelewa
na waliokuwa walimu wao kipindi hiko wakiwa wanasoma shule hapo na
kupata nafasi ya kuonyeshwa sehemu mbalimbali za shule hiyo huku
waliokuwa wanafunzi katika shule wakipata nafasi pia ya Kuzungumza
machache na wanafunzi wanaoendelea na masomo katika shule hiyo na kuweza
kuwasaidia vifaa vya michezo kama mipira huku wakipanda miti kwaajili
ya kumbukumbu.
Waliokuwa
wanafunzi wa shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza nchini
waliweza kutoa miche 30 ya miti kwaajili ya kupandwa shule hapo huku
wanafunzi wakishukuru kwa kupokea mipira kama zawadi kutoka kwa kaka na
dada zao waliotangulia shuleni hapo.
Akizungumza
na waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo Kaka Mkuu msaidizi alisema “Kwa
niaba ya wanafunzi wenzangu napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kaka
na dada zetu ambao mliweza kusoma hapa na kuamua kuja kutusalimia na
kututia moyo, Kiukweli tumefarijika sana na tunaomba muendelea kuja
shule hapa muda wowote ule kwa maana tumejisikia faraja sana kuwaona na
vilevile tunapenda kushukuru kwa kutuletea Zawadi ya Mipira hii,
tunasema asanteni sana”
Mara
baada ya waliokuwa wanafunzi wa shule hiyo kutembelea sehemu mbalimbali
za shule na kuzungumza na wanafunzi wa shuleni hapo waliweza kupata
chakula cha mchana na waliokuwa walimu wao kipindi wanasoma na kuweza
kubadilishana mawazo huku walimu wakishukuru sana na kusema wamefurahi
sana kuwaona wanafunzi hao kwa maana ni miaka mingi sana imepita tokea
wengi wao wahitimu masomo yao hapo shule.
Shule
ya sekondari ya Bwawani ilikua ikiitwa Ubena kabla ya kubadilishwa jina
na Kuitwa Bwawani kutokana na mantiki ya kuwa shule ya kufundisha raia
peke yao ambapo awali ilikuwa ni shule kwaajili ya kuendeleza elimu kwa
askari wake wa jeshi la magereza, Mnamo mwaka 2002 jina lilibadilika
kutoka Shule ya Sekondari Ubena na kuitwa Bwawani ambapo sasa ilianza
kupokea wanafunzi raia ambao kwa mara ya kwanza usajili wa wanafunzi
raia ulianza mwaka 2001. Katika kipindi hiko shule ya Bwawani ilikuwa ni
shule yenye Kidato cha Kwanza mpaka Cha nne ambapo sasa shule hiyo ina
kidato cha Tano na cha sita.
No comments:
Post a Comment