Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, July 27, 2016

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AMEZUNGUMZA NA WAUMINI WA KANISA LA TAG MELINZE


 WAIMBAJI WA KWAYA YA TWENDE KWA NANI WAKITUMBUIZA

 MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG MELINZE CEFANIA TWEVE AKIZUNGUMZA NA WAUMINI WA KANISA HILO
 HAPA MCHUNGAJI TWEVE  MWENYE TAI UPANDE WA KUSHOTO ,ANAYEFUATA NI KATIBU TAWALA WILAYA YA NJOMBE JACKSON CHOTA ,WA TATU KUTOKA KUSHOTO NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI,NA WA MWISHO NI ANNA WIKETYE  KATIBU TAWALA MSAIDIZI WILAYA YA NJOMBE WAKIWA KWENYE KANISA LA TANZANIA ASSEMBLES OF GOD MELINZE LEO.
 KATIBU TAWALA AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUMKARIBISHA MKUU WA WILAYA
 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE LUTH MSAFIRI AKIZUNGUMZA NA WAUMINI WA KANISA HILO

 HAPA MCHUNGAJI ANAMSINDIKIZA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI  ALIOONGOZANA  NAO




Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Luth Msafiri  Leo Ameanza Ziara Yake Ya Kutembelea Taasisi  Za Serikali Na

Za Watu Binafsi  Kwa Lengo La Kujitambulisha  Akianza Na Makanisa 11 Ya Njombe Mjini Ambapo Akiwa Katika Kanisa La TAG  Mkuu Huyo Wa  Wilaya  Ametaka Waumini Na Wananchi Kuwapuuza Baadhi Ya Watu Wanaoendekeza Siasa Kipindi Cha Kazi.

Kauli Hiyo Ameitoa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Luth Msafiri Hii Leo Wakati Akizungumza Na  Waumini Wa Kanisa La TAG Kwenye Kongamano La Wanaume  Na Kusema Kuwa Siasa Zinakwamisha Maendeleo Kwa Jamii  Hivyo Wanapaswa Kuepukana Na  Wanaoendekeza Siasa  Swala La Siasa Badala Yake Waongeze Juhudi Katika Uzarishaji  Mali Na Kwa Manufaa Yao Na Taifa.

Aidha Bi.Msafiri  Ameomba  Waumini  Wa Makanisa Mbalimbali  Wilayani Njombe Kuendelea Kudumisha Amani Na Utulivu    Ambayo Inategemewa Kuanzia Kwenye Makanisa  Huku Akiomba Wachungaji  Kuhimiza Waumini Kuacha Kuendelea Na Siasa Kwani Wametoka Kwenye Kipindi Kigumu Cha Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka Jana.

Bi.Msafiri Amesema Chanzo Cha Amani Na Utulivu Ni Makanisa  Hivyo  Wachungaji Wanatakiwa Kutilia Mkazo Kuhubiri Amani Kila Siku  Huku Akiomba Wananchi Na Waumini Kujenga Mazoea Ya Kuhudhuria Mikutano   Inayoitishwa Na Viongozi Wa Serikali Ili Kupeana  Utaratibu Na Mabadiliko Ambayo Wamejiwekea Au Kiongozi Wa Wilaya Ujumbe Atakaohitaji Kuwafikishia.

Kwa Upande Wake Mchungaji  Wa Kanisa La TAG Melinze Cefania Tweve  Amemshukuru Mchungaji Huyo Kwa Kuwatembelea Na Kutoa Ujumbe Huo Ambapo Ameahidi Kuufanyia Kazi Kwa Kuwaelimisha Waumini Kuhusiana Na  Umuhimu Wa Kutekeleza Majukumu Yao  Kwa Serikali  Na Kutaka Kumutegemea Mungu Zaidi Katika Kazi Zote Zinazofanyika.

Awali Akimkaribisha Mkuu Wa Wilaya Huyo Katibu Tawala Wilaya Ya Njombe Jackson Chota   Alisema  Ziara Hiyo Imelenga Kufahamiana Na Taasisi Mbalimbali Za Serikali Na Za Watu Binafsi   Ili Mkuu Wa Wilaya  Ashirikiane Vizuri Katika Kutekeleza Majukumu Ya Serikali Kwenye Halmashauri Yake Ya Njombe  Na Kwamba Wakati Mwingine Atakuwa Anaongozana Na Wataalamu Wa  Halmashauri Husika Kwenye Mikutano Ya Hadhara.


No comments:

Post a Comment