Mwenyekiti
aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa
chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia
mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa
rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio ziapatazo
2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.
Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete
akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi
(CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na
Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka
kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya
Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi
(CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na
Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka
kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
Makamu
Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John
Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka
10,pichani katia anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt
Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti
Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama
hicho kwa miaka 10.
Mwenyekiti
mpya wa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia
mbele ya Wajumbe wa Mkutano mkuu Maalum wa chama cha CCM mara baada ya
kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti
Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama
hicho kwa miaka 10.
Mwenyekiti
Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John
Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama
hicho kwa miaka kumi.
Baadhi
ya Wajumbe wa Mkutano mkuu maalum wa CCM wakipiga kura kumchagua
Mwenyekiti mpya wa chama hicho ambaye anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.Mkutano huo ukiongozwa
na Mwenyekiti wa CCM ambaye anamaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne
Dkt Jakaya Kikwete amekiongoza chama hicho kwa Miaka 10 na leo anawaaga
wanachama na wajumbe mbalimbali wa chama cha Mapinduzi jioni ya leo
mjini Dodoma.
Wajumbe kutoka mikoa mablimbali wakipiga kura
Wajumbe wameisha piga kura na mabox yakiwa tayari kuhesabiwa na baadae kutolewa majibu
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh Al Hassan Mwinyi akipiga kura ya kumchagua Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi jioni ya leo
Baadhi
ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri kwenye mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Dodoma
Convetion Center,uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma
Mwenyekiti
wa CCM ambaye amemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya
Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wajumbe mkuu wa Mkutano mkuu wa
CCM,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mh Kassim
Majaliwa kabla ya matokeo ya kumpata Mwenyekiti wa chama hicho
hayajatangazwa rasmi jioni ya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti
Mstaafu aliyemaliza muda wake leo,Dkt Jakaya Kikwete pamoja na
Mwenyekiti mteule,Rais Dkt John Pombe Magufuli
Kada Mkongwe wa chama cha CCM Mzee Makamba akimpongeza Mpendazoe kwa kurejea CCM.
No comments:
Post a Comment