Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, July 5, 2016

EWURA KUTANGAZA BEI ELEKEZI YA MAFUTA KESHO JULAI 6,IKIWA LEO WAKAZI WA NJOMBE WAMEKABILIWA NA UHABA WA MAFUTA KWA TAKRIBANI SAA TANO KITUO KIMOJA TU KILIKUWA KINATOA HUDUMA


NJOMBE

Mamlaka Ya Udhibiti Wa Nishati Ya Mafuta Na Maji Nchini EWURA Kesho Inatarajia Kutoa Bei Elekezi Kwa Wauzaji Wa Nishati Ya Mafuta Ambapo Wafanyabiashara Wa Mafuta Mkoa Wa Njombe Wameshauriwa Kutoficha Mafuta  Kwa Lengo La Kusubiria EWURA Ipandishe Bei  Kwani Kufanya Hivyo Ni Kukiuka Kanuni Na Sheria Za Biashara.

Rai Hiyo Imetolewa Na Afisa Biashara Wa Mkoa Wa Njombe  Musa Lwalilino  Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Tatizo La Kukosekana Kwa Mafuta Ya Petrol  Katika Baadhi Ya Vituo  Vya Mafuta  Ambapo Kati Ya Vituo Saba Vya Mafuta Vilivyopo Njombe Mjini Ni Kituo Kimoja Cha Kwa Mwalabu Ndicho Kilichokuwa Kinaendelea Kutoa Huduma Kwa Wateja.

Bwana Lwalilino Amesema Kuwa Tatizo La Kukosekana Kwa Mafuta Njombe Mjini Kumetokana Na Meli Kuchelewa  Kufikisha Mafuta Jijini Dar Es Salaamu  Jambo Ambalo Limesababisha Msongamano Wa Magari Yanayokwenda Mikoani  Na Matokeo Yake Ni Kukosekana Kwa Mafuta Maeneo Mbalimbali  Ya Mikoa Nchini.

Aidha Lwalilino Amekemea Tabia Ya Baadhi Ya Wamiliki Wa  Vituo Vya Mafuta  Ambao Wanahifadhi Badala Ya Kuuza  Kwaajili Ya Kusubilia Bei Elekezi Itolewa Na EWURA Na Kusema Kuwa Hatua Kali Zitachukuliwa Kwa Watakao Bainika Kukiuka Ikiwemo Kufutiwa  Leseni Zao Za Biashara Na Kufikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma Zitakazokuwa Zinawakabili.

Akizungumza Na Uplands Fm Mkurugenzi Wa  Kituo Cha Mafuta Chaugingi Ahamed Kaserehe  Amesema  Mafuta Yameadimika Kwa  Siku Mbili  Jijini Dar Es Salaamu Ambapo Yeye Alikuwa Na Mafuta Ya Ziada Ndiyo Anayoyauza  Wakati Vituo Vingine Vikiwa Havina Mafuta  Huku Akisema Kwa Mujibu Wa Leseni Ya EWURA Analazimika Kuuza Na Kuitaka Serikali Kufuatili Wauzaji Mafuta Ya Jumla Jijini Dar  Es Salaamu Ili Kuondoa Adhaa Inayowakabili Wananchi.

Elika Mlope Ni Accountant  Wa Kituo Cha Mafuta Gapical  Amesema Wao Wameishiwa Tangu Jana Jioni  Na Kuwahakikishia Wateja Kuwa Kufikia Mchana Wa Leo Yatakuwa Yamekwisha Wasili Njombe Na Huduma Kituo Hicho Kitaendelea Kutoa Huduma Ya Mafuta Ambapo Hadi Tunaingia Mitamboni Mafuta Yalikuwa Yameanza Kutolewa Kwa Baadhi Ya Vituo  Vilivyokuwa Havitowi Mjini Njombe.

Diwani Wa Kata Ya Ramadhani Geoge Sanga  Na Diwani Mstaafu Wa  Kata Ya Imalinyi  Enock Kiswaga Wakiwa Miongoni Mwa Wahanga  Wa Kukosa Mafuta Wametaka Wafanyabiashara Wa Mafuta Kuweka Mafuta Ya Kutosha Huku EWURA   Wakitakiwa Kufuatilia Baadhi Ya Wafanyabiashara Wanaosababisha Kukosekana Kwa Mafuta Kwa Makusudi Na Kuwachukulia Hatua Za Kisheria.

Awali Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Wamiliki  Na Madereva Wa Pikipiki Na Magari Walilalamikia Kukosekana Kwa Mafuta  Kwa Muda Wa Masaa Takribani Sita  Kutokana Na Mafuta Kucheloewa Kufika Jijini Dar Es Salaamu Baada Ya Meli Kuchelewa  Kufikisha Ambapo Wameitaka Serikali  Kuboresha Usimamizi Wake Kupunguza Kero Kwao.

No comments:

Post a Comment