KAULI YA KATIBU TAWALA WILAYA YA NJOMBE JACKSON CHOTA AMBAYO AMEITOA WAKATI AKIWA MGENI RASMI KWENYE MKUTANO WA WALEMAVU WA VIUNGO
MWENYEKITI WA WALEMAVU WA VIUNGO MBALIMBALI MKOA WA NJOMBE JACKSON FIHANGA
HAWA NI BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA MKOA YA WALEMAVU MKOANI NJOMBE
Viongozi Wa Taasisi Za Serikali Na Watu Binafsi Wilayani Njombe Wametakiwa Kuzingatia Kanuni Na Taratibu Za Utawala Bora Kwa Kuitisha Vikao Kwa Mujibu Wa Sheria Kwaajili Ya Kujadili Maendeleo Ya Usimamizi Wa Miradi Inayotekelezwa Katika Maeneo Yao Ili Kuondoa Migogoro Ambayo Imekuwa Ikijitokeza Hususani Ile Inayohusu Maswala Ya Fedha.
Rai Hiyo Imetolewa Na Katibu Tawala Wilaya Ya Njombe Jackson Chota Wakati Akizungumza Na Wajumbe Wa Kamati Tendaji Ya Walemavu Mkoa Wa Njombe Ambayo Imekutana Katika Ofisi Ya Chama Cha Walemavu Mkoa Kujadili Maendeleo Ya Miradi Na Changamoto Zinazowakabili Walemavu Hao Pamoja Na Kushawishi Walemavu Wengine Walioko Nyumbani Kuwa Kitu Kimoja.
Katibu Tawala Chota Amesema Migogoro Mingi Huanzia Kwenye Vipengele Vinavyo Husu Fedha Baada Ya Wajumbe Na Wananchi Kutokuwa Na Imani Na Usimamizi Wake NA kusababisha Kuwepo Kwa Masikitiko Na Maneno Yenye Kulaumu Upande Wa Uongozi Kutokana Na Vikao Na Mikutano Kutoitishwa Kwa Lengo La Kila Mmoja Kupewa Nafasi Ya Kuhoji Na Kushauri Namna Wanavyoweza Kutekeleza Miradi.
Akisoma Risala Ya Chama Cha Walemavu CHAWATA Mkoa Wa Njombe Mwenyekiti Wa Chama Hicho Jackson Fihanga Amesema Chama Hicho Kilianzishwa Mwaka 1982 Kufuatia Tangazo La Umoja Wa Mataifa Kutangaza Kuwa Mwaka 1981 Ni Mwaka Wa Kimataifa Wa Walemavu Na Serikali Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ililidhia Tangazo Hilo Na Kuhimiza Kuanzishwa Kwa Vyama Vya Walemavu.
Fihanga Amesema CHAWATA Njombe Imekuwa Ikishawishi Walemavu Wengine Kuwa Pamoja,Kuwapa Ushauri Nasaha Walemavu Kuukubali Ulemavu Wao Na Kuunda Matawi Katika Wilaya Na Vijiji Ambapo Chawata Na Chama Cha Wasiyoona Njombe Vilifanikiwa Kuanzisha Mradi Wa Duka ,Kununua Gari Na Nyumba Huku Kikishindwa Kupata Viongozi Wa Taifa Kutokana Na Mkutano Wa Uchaguzi Kutoitishwa.
Baadhi Ya Walemavu Mkoa Wa Njombe Wameiomba Serikali Kuingilia Kati Kusimamia Uchaguzi Wa Viongozi Wa Kitaifa Wa Walemavu Na Kwamba Wamekuwa Wakilalamikia Kaimu Mwenyekiti Wa Chama Hicho Ili Aitishe Mkutano Mkuu Wa Taifa Wafanye Uchaguzi Wa Viongozi Wao Lakini Amekuwa Hafanyi Hivyo.
No comments:
Post a Comment