MWENYEKITI WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO MKOA WA NJOMBE ALLY MHAGAMA MARUFU SAGASAGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI
KAIMU KATIBU WA ACT MKOA WA NJOMBE NELSON KYANDO AKITOLEA UFAFANUZI JUU YA SIKU HIYO
Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa Wa Njombe Kimelazimika Kuahirisha Sherehe Za Kutimiza Miaka Miwili Ya Kuanzishwa Kwa Chama Hicho Mkoa Wa Njombe Kutokana Na Sababu Mbalimbali Ikiwemo Baadhi Ya Viongozi Wa Chama Kuwa Na Majukumu Mengine Ambapo Kilele Cha Maadhimisho Hayo Kitaifa Yanafanyika Mkuranga Mkoani Pwani.
Akizungumza Na Uplands Fm Mwenyekiti Wa Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa Wa Njombe Ally Mhagama Maarufu Kama Sagasaga Amesema Chama Hicho Kwa Mkoa Wake Kinatarajia Kufanya Maadhimisho Hayo Mnamo Mei 18 Mwaka Huu Siku Ya Jumamosi Ya Wiki Ijayo Ambapo Maadhimisho Hayo Yatakwenda Sambamba Na Uhamasishaji Wananchi Kuchangia Damu Salama Kwaajili Ya Wagonjwa Wa Hospitali Ya Kibena.
Aidha Bwana Mhagama Amesema Jitihada Za Chama Hicho Kuhamasisha Wanachama Na Wananchi Mkoa Wa Njombe Bado Zinaendelea Kwani Wameanzisha Zoezi Hilo Baada Ya Kutambua Uwepo Wa Changamoto Ya Kukosekana Kwa Damu Salaama Katika Hospitali Zilizopo Nchini Na Kuataka Wadau Wengine Kuunga Mkono Jitihada Zitakazofanyika Na Chama Hicho Za Kuchangia Damu Salaama.
Kwa Upande Wake Kaimu Katibu Wa Chama Cha ACT Wazalendo Mkoa Wa Njombe Nelson Kyando Amesema Chama Hicho Kinatarajia Kuwafikia Wananchi Wa Maeneo Mbalimbali Yakiwemo Ya Vijijini Ili Kuiambia Jamii Juu Ya Makusudio Ya Chama Hicho Juu Ya Kuhimiza Maendeleo Kwa Kila Mwananchi Pamoja Na Kuongeza Idadi Ya Wanachama Na Kwamba Chama Hicho Kitasikiliza Kero Zao.
Kyando Amesema Kwa Mujibu Wa Katiba Ya Chama Hicho Wanatarajia Kupeleka Mahitaji Mbalimbali Kwa Watu Wasiyojiweza Kwa Kuwasaidia Mahitaji Ya Msingi Ili Kutoa Mfano Kwa Wananchi Na Wadau Wengine Kujenga Mazoea Ya Kusaidia Makundi Hayo Yakiwemo Ya Wazee Huku Akitaja Misingi Ya Katiba Ya Chama Hicho Kwani Miongoni Ni Uwajibikaji Na Usawa Pamoja Na Uadilifu.
No comments:
Post a Comment